A

A

[PHOTO'S]MAMIA WAHUDHURIA MAZISHI YA WAZIRI MGIMWA LEO HUKO IRINGA,

Maelfu ya wakazi wa mkoa wa Iringa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa na Serikali wakiongozwa na Rais Dr Jakaya Kikwete wameshiriki katika mazishi ya aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kalenga na waziri wa fedha Dr Wiliam Mgimw

Katika mazishi hayo yaliyofanyika leo kijiji kwake Magunga jimbo la Kalenga wananchi mbali mbali walionyesha kujipanga barabarani kutoka Manispaa ya Iringa hadi kijiji ni kwake huku wakiupungia mkono msafara wa rais Kikwete na baadhi yao wakilazimika kutumia usafiri wa baiskeli na pikipiki kwenda katika mazishi hayo.

Akitoa shukrani za familia kwa niaba ya familia mtoto wa marehemu, Dr Mgimwa Godfrey Mgimwa, aliishukuru Serikali kwa jinsi ambavyo ilivyohangaika kumuuguza baba yake na kutoa wosia mzito wa marehemu Dr Mgimwa ambao alimtaka kuufikisha kwa Rais Kikwete..

Alisema katika uhai wake kabla ya kifo chake, ikiwa ni siku tano kabla hajafariki, Dr. Mgimwa alimwita na kumtaka kufikisha shukrani zake kwa Rais Kikwete kwa kumtembelea mara mbili Hospital alipokuwa amelazwa pamoja na Spika wa bunge Anne Makinda .

"Baba kabla ya kufa aliniachia wosia huo juu ya wana Kalenga kwa kuwashukuru kwa ushirikiano wao na alipenda kuona Kalenga inakuwa na maendeleo zaidi,” alisema Dr. Godfrey Mgimwa.

Kwa upande wake waziri Mkuu Pinda alisema kuwa Serikali imepata pigo kubwa juu ya kifo hicho na kuwa bado Serikali itaendelea kuwa karibu na familia ya Dr Mgimwa na pale penye tatizo isisite kuwasiliana.

Kwa upande wa Spika wa Bunge, Anne Makinda, yeye alisema kuwa Bunge limempoteza kiongozi na mbunge aliyependa kutumia nafasi yake kwa ajili ya Taifa na kuwa kamwe mchango wake hawataacha kuukumbuka.
na mzee wa matukio daima.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako