Ndesamburo amkingia kifua Lowassa
“Hata huku kwenye vyama vyetu CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi wapo wanaotuvuruga, lakini sasa hivi habari ya mjini ni Lowassa, Lowassa… kama kweli hatupendezwi na hali hiyo tuwanyooshee wote basi, kama hatuwezi wamwache aendeleze ndoto yake. The best way to predict the future is to invent it,” aliongeza Ndesamburo. Alisema kwa mantiki hiyo, njia sahihi aliyoitumia Lowassa ya kutamka hadharani kusudio la kukamilisha majaliwa ya ndoto zake, ni namna alivyonyambulisha kile kinachoshabihi mawazo yake ya muda mrefu ya kuwatumikia Watanzania wenzake. Ndesamburo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kilimanjaro, alisema haijalishi kwamba yeye ni mpinzani wa CCM, lakini kumshambulia Lowassa peke yake, ingali kuna vinara wengine wanaokigawa chama chao si haki. “Haijalishi ya kuwa mimi ni mpinzani na najua hata wao wanalijua hilo kwamba Ndesamburo ni nguli wa siasa za mageuzi ya kifikra katika taifa, nasema wawatizame na hao wengine wanaopita huko huko makanisani na misikitini kujitangaza kwa kisingizio cha kualikwa katika harambee,” alisema Ndesamburo. Hata hivyo, Ndesamburo amewaomba Watanzania kuwachagua wagombea wa CHADEMA watakaopitishwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu kwa kuwataka kuwakataa watu wanaotaka kuwachagulia viongozi wa kuwaongoza. Katika siku za karibuni kumekuwa na matamko ya makatazo kutoka kwa viongozi wa CCM wakiwemo wale wa jumuiya, yakimtaka waziri huyo mstaafu kuacha kuendelea na kile kinachodaiwa kuwa kampeni za chini kwa chini za kuusaka urais.
TANZANIA DAIMA