Ingekuwa ni msanii mwingine ungesikia ameshapotea katika ramani hii
ya muziki kutokana na ukimya wake ila siyo Ali kiba,akiwa ndiye nominee
wa tuzo za KORA 2012,mwaka jana ni mwaka ambao msani huyu aliweza kukaa
kimya kwa muda mrefu huku watu wengi wakihisi kuwa ameacha muziki
kabisa,ila si hivyo,Kati ya wasanii wa hapa Bongo wanaoheshimika sana
basi Ali Kiba anapewa nafasi ya kipekee kutokana n uwezo wake wa kuimba
na kule kutokuwa na drama nyingi za hapa na pale kama kawaida ya wasanii
wengi wa muziki huu wa Bongo hasa pale wanapopata umaarufu,kuongelea
kuhusu Ali kiba unaweza kusema ni mfano wa msanii wa Bongo fleva,ni moja
ya msanii ambaye nyimbo zake zimeweza kukaa muda mrefu bila kuisha ile
ladha ya muziki wake.
Mbali na ukimya alionao wa mwaka mzima wa jana,ila bado hata wasanii
wenzake wamekuwa wakimkubali sana,kutokana na uwezo mkubwa wa kuimba
aliokuwa nao,kwa wasanii wanaochipukia,alikiba amekuwa kama reference
point,yani wasanii wanangalia wafanye muziki ili wafike level kama zake
Ali Kiba,ikiwa ni pamoja na kuwa na ndoto zakufanya kazi na msanii
huyu.Mwishoni mwa mwaka jana msanii chipukizi Naylee alifunguka na
kusema kuwa nyimbo za Ali Kiba ndizo zilizomfanya aweze kupata moyo na
kuingia katika maswala haya ya muziki na kuwa na ndoto siku moja kufanya
kazi na Ali Kiba.huyu ni mmoja tu ya wasanii chipukizi mwenye ndoto za
kufanya kazi,hivyo mbali na kuwa kimya kwa muda Ali kiba bado amekuwa
kwenye ndoto ya kila msanii kutaka kufanya nae kazi.
Nyimbo za Ali Kiba,kutokana na
wadau mbali mbali waishio nje ya
nchi,wanasema kuwa hupigwa sana huko nje ya nchi,moja ya nchi zinazopiga
sana nyimbo za ali kiba ni huko Muscat,Inasemekana ni msanii wa bongo
fleva anayesikilizwa kuliko msanii yeyote yule,hata kwa wale wasiojua
kiswahili wamekuwa wakisikiliza nyimbo zake,..unaweza kufananisha haya
yote na nyimbo za michael jackson hivi leo,sidhani kama watu wengi
wanaopenda nyimbo zake wanajua kingereza,ila bado wanasikiliza na
kuzicheza.Ukirudi hapa East Africa ali kiba bado anacheza role kubwa
kwenye list ya kila mmoja ya nyimbo azipendazo,na huko nchini kenya
mbali na kutotoa hit single kwa kipindi cha muda mrefu,ni moja ya msanii
anayeongoza kwa nyimbo zake kuwa requested sana,hii yote inaonyesha
kuwa bado nyimbo zake zinapendwa sana na watu,haijalishi nyimbo ni ya
mwaka gani.
Ni moja ya msanii aliyekuwa poa sana kusaidia wasanii wadogo
wanaochipukia na hivyo kuwa kioo cha msanii ambaye anajali sana na
kuheshimu kazi za mtu mwingine,ukiongelea ali kiba ni msanii ambaye yuko
social sana na ameweza kusaidia wasani wengi sana wanaochipukia
kimawazo na hata kufanya nao collabo katika nyimbo zao,imekuwa kawaida
sana kwa wasanii wakubwa baada ya kupata umaarufu kusahau walipotoka
kuwa wao pia mwanzo walikuwa chipukizi wakitafuta njia yakutokea kwa
kukataa kabisa kufanya collabo na wasanii wachanga,but kwa Ali kiba ni
tofauti kabisa,mbali na umaarufu wake mkubwa amekuwa msaada mkubwa kwa
wasanii wanaochipukia,Talking about Ali Kiba ni moja ya msanii mkubwa
wakuigwa.
Vibe
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako