A

A

Mchezaji Boniface Njohole Afariki Dunia.TFF yatoa Rambirambi

 
TFF YATOA RAMBIRAMBI MSIBA WA MCHEZAJI BONIFACE NJOHOLE
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa zamani wa timu ya Reli Morogoro, Boniface Njohole kilichotokea jana (Januari 12 mwaka huu) mkoani Morogoro.
Njohole ambaye alikuwa mjumbe wa Kamati ya Ufundi na Mashindano ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA) hadi umauti unamkuta anatarajia kuzikwa kesho (Januari 14 mwaka huu) kijijini kwao Mngeta wilayani Ifakara.
Msiba huu ni mkubwa kwa jamii ya mpira wa miguu kwani alitoa mchango akiwa mchezaji, kocha na kiongozi kwa nyakati tofauti, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Njohole, klabu ya Reli na MRFA na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito. Pia TFF itatoa ubani wa sh. 200,000 kwa familia ya marehemu kama rambirambi zake.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina