Na Faustine Ruta, Bukoba
TIMU ya Mbeya City leo imeanza msimu wa pili vyema baada ya kuifungia
Kagera Sugar kwenye uwanja wao wa nyumbani kaitaba bao 1-0. Kipindi cha
kwanza kilimalizika kikiwa hakuna timu iliyokuwa imeziona nyavu za
mwenzake hivyo zikalazimika kwenda mapumziko zikiwa 0-0, Huku kipa wa
Kagera Sugar Hannington akiwa hoi kwa kuumia mguu baada ya kuachia frii
kiki na kushtuka mguu na kulazimika kutolewa nje katika kipindi hicho
cha kwanza. Kipindi cha pili dakika ya 72 Mbeya City wamepata bao
kupitia mchezaji wao Richard Peter aliyekuwa amevaa jezi no. 13
mgongoni.
Kikosi kilichoanza cha Mbeya City
Patashika kuutafuta mpira
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako