Timu ya Azam Fc na viongozi wake ni mfano wa kuigwa kwa nchi nzima ya
Tanzania, Siwezi kuzitaja timu kubwa za Yanga na Simba maana huko ni
uonzo mtupu. Nimesema nchi nikiwa na maana kukiwa na sehemu maalum za
michezo kama ilivyo kwa Azam Complex tutashindwaje kupata wachezaji
wazuri wenye nidhamu na moyo wa kujituma?. Na tukawa na timu ya taifa
ambayo haitakuwa kichwa cha mwenda wazimu?. Hongera sana Azam na
viongozi wake kwa kuwa na uwanja mzuri na wenye kila kitu kinachowafanya
wachezaji wajisikie kuwa wako nyumbani.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako