A

A

Maafisa Marekani waharibu mayai 103 aliyokutwa nayo abiria aliyetokea Kenya


Phoenix, Az — Msafiri mmoja aliyekuwa akisafiri kwa ndege kutokea Kenya via London amejikuta akipewa onyo la kutokujaribu kuthubutu tena kubeba mayai kwenye ndege wakati mwingine atakaposafiri, baada ya kukutwa na mayai 103 ya ndege pale mizigo yake ilipokaguliwa na maafisa katika kiwanja cha ndege cha Sky Harbor cha jijini Phoenix jimboni Arizona.

Maafisa wa Kilimo katika kiwanja hicho wenye jukumu la kukagua aina ya vyakula, mbegu na mazao yanayoingizwa nchini
Marekani ili kuzuia baadhi ya ambayo hayatakiwi kwa kuwa yanaweza kuleta madhara ya magonjwa na wadudu kwa mimea na mazao mengine, waliyazuia mayai hayo kwa mujibu wa kifungu cha “9 CFR 94 Prohibited and Restricted Importations of Animals and Animal Products” walisema mwanamke huyo alipohojiwa sababu ya kubeba mayai hayo aliyokuwa ameyahifadhi kwenye kisanduku cha plastiki, alijibu kuwa ni kwa ajili ya tiba yake ya moyo.

Maafisa hao waliyaharibu mayai hayo bila

kumpiga faini na kumfahamisha kuwa wakati ujao asafiripo, anapaswa kujaza ukweli katika kadi maalumu inayouliza endapo msafiri amebeba mazao yoyote ya kilimo ama chakula, la sivyo atapigwa faini kwa mujibu wa sheria.

---

Binafsi niliwahi kulipishwa faini ya $300 kwa kuwa nilikuwa nimebeba viungo vya chakula nilivyonunua Zanzibar, miongoni mlikuwemo na viungo ambavyo vilihesabika kama mizizi ambayo ingeweza kuzaa endapo ingeoteshwa na hivyo kosa kubwa lilikuwa kutokujaza kwenye karatasi maalumu aina ya mazao niliyobeba. Vilivyonitoa faini vilikuwa vitatu - mizizi ya manjano (inafanana na ya tangawizi), jani bichi la aloe vera lenye mizizi (hivyo ligeweza kuota) na kingine nimesahau.

Nadhani pia hii hurekodiwa moja kwa moja kwenye faili la mhusika kwani wakati mwingine nikitoka kwingineko nilijisahau nikawa na chupa yenye soda aina ya Sprite zaidi ya mililita 30 zinazoruhusiwa, hivyo nikaitwa pembeni na kupekuliwa na kupewa onyo, soda ile ikachukuliwa na kutupwa kwenye kapu la taka.

Tangu wakati huo nimekuwa makini katika kupanga na kuhakika vitu ninavyosafiri navyo na kuhakikisha ninajaza fomu maalumu ku-declare nilichofungasha

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako