A

A

Kuhusu Watanzania Wawili Kumwagiwa Tindikali Oman,HIi ndio taarifa ya Kweli

 

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya watanzania Oman Ndugu Hassan Mtonga( Aliesimama) akiongea na watanzania katika mkutano mkuu wa Jumuiya watanzania nchini Oman uliofanyika Muscat, Oman Ijumaa tarehe 17 Januari 2014.
 
 ******
Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Oman (Tanzania Club in Oman-TANCO) ilifanya mkutano wake mkuu hapo Ijumaa tarehe 17.01.2014 mkutano uliohudhuriwa na watanzania jumla ya 150 wanaoishi na kufanya kazi nchini Oman.
 Katika Mkutano huo Mwenyekiti wa TANCO ndugu Hassan Wazeer Mtonga alitumia mkusanyiko huo kutafuta usahihi wa habari zilizoenea pamoja na picha zikionyesha wanawake wawili wakiwa wameungua na kudai kuwa ni wadada wakitanzania na kuwa wamefanyiwa ukatili huu na mabosi wao wa kioman.

Ndugu mtonga alieleza kuwa

alizipata taarifa hizo nayeye kwa nafasi yake ya Uenyekiti aliziwasilisha Ubalozi wa Tanzania nchini Oman ambao nao walizifanyia kazi kushirikiana na Serikali ya Oman kupitia polisi, hospital na viwanja vya ndege, lakini taarifa hazikuonesha kuwepo kwa tukio hilo na kuthibitisha kuwa ni uzushi na uongo kwani hawakuweza kupata majina ya watanzania hao, waajiri wao na mazingira ya mashambulio hayo.
Ndugu Mtonga aliwaomba watanzania wote waliohudhuria Mkutano huo ambaye anataarifa sahihi kuhusu matukio hayo aziwasilishe , lakini hakuna hata mmoja aliekiri kuwa na taarifa kamili zaidi ya kupokea picha hizo kupitia mtandao wa Whatsapp.
Mwenyekiti alisisitiza kuwa habari ile si ya kweli na kwamba ni uzushi usio na misingi yeyote ambao unaweza kuwa na athari kubwa katika mahusiano ya nchi.
Mwenyekiti alieleza kuwa habari hii ya uvumi wa kuunguzwa na kumwagiwa tindikali kwa watanzania haikupokelewa vizuri na wenyeji wetu waoman na kuwa inatishia kuharibu uhusiano wa kundugu na kihistoria uliopo baina ya Tanzania na Oman na pia watanzania na waoman kwa kupelekea kuzuiwa kwa watanzania kuja Oman kufanya kazi na hivyo kushindwa kutumia fursa za ajira zinazopatikana OmanMwenyekiti aliwaasa watanzania kuwa makini na matumizi ya mtandao na kuepusha kutumia mitandao kusambaza habari ambazo si za kweli. Aliwaomba kuwa habari yeyote inayomuhusu mtanzania mahala pa kuanzia ni ubalozini au kwenye Jumuiya ya Watanzania nchini Oman.
Mwenyekiti pia aliwasihi wa Tanzania kufanya kazi kwa juhudi, maarifa na nidhamu ili kuijengea sifa nzuri Tanzania. Aliwakumbusha Usia wa Rais Jakaya Kikwete alipokutana na watanzania wanaoishi Oman wakati alipotembelea Oman mwaa 2012 alipowausia watanzania kuwa raia wema na kujiepusha na vetendo vya uvunjaji sheria za nchi wanamoishi.

chanzo:BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako