Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, anatarajia kukutana na Kamati
Kuu ya shirikisho la bodaboda Saccos kwa ajili ya ufunguzi wa Saccos
hiyo.
Ufunguzi huo unatarajia kufanyika kesho jijini Dar es Salaam, lengo likiwa ni pamoja na kuwakwamua kiuchumi madereva bodaboda nchini.
Ofisa habari wa Chama cha bodaboda mkoa wa Ilala, Abdallah Bakari, alimshukuru Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli (CCM), kwa kutambua umuhimu na uwepo wa bodaboda na kwamba ni mfano wa kuigwa na viongozi wengine.
Bakari amewataka viongozi wengine kuiga mfano huo na kuwasaidia vijana ili kuwawezesha kuinua vipato vyao na kuwawezesha pia kimiliki pikipiki na kuondoa matatizo yanayojitokeza.
Pia, ameziomba asasi na watu mbalimbali kuwasaidia madereva bodaboda walioko hospitalini kutokana na ajali, kupata matibabu ili waweze kurejea kazini kwani wamekuwa wakikaa kwa kipindi kirefu bila kupatiwa matibabu na wengine kufariki.
Madereva hao pia wametakiwa kuzingatia sheria na kanuni za barabara ili kupunguza ajali.

No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako