Hii
ni interview ya kwanza ya mwigizaji Kajala, yani ndio kwa mara ya
kwanza kahojiwa kwenye chombo cha habari (Exclusive on millardayo.com)
baada ya kumiliki headlines kwa ishu zake tatu ambazo ni kuchukua mume
wa mtu, kudaiwa kukamatwa na dawa za kulevya na safari yake kwenda
China.
Yafuatayo ni maswali ya millardayo.com nyumbani kwake Dar es salaam.
millardayo.com : Ni kweli kuhusu hii ya mume wa mtu?
Kajala: Hapana, niliambiwa mtu wa kwanza kuandika hii alikua mtu wa
blog ndio magazeti na mitandao mingine ikafata ila sio kweli…
sikufatilia manake ukweli naujua mwenyewe, niliumia na hata mama yangu
aliumia na aliniuliza.
Kwenda club au kukutana na
mtu na kupiga nae picha sio kwamba umeiba
mume wa mtu, huyo dada kama kweli yule angekua mume wake angenifata
manake haya kuniona hivi hajawahi… yeye yuko Hongkong mi niko China
ananiambia nimeiba mume wake…. huyu Mwanaume anaishi hukohuko, China
nilikwenda mwenyewe na wala sio kwamba nimetoka nae Tanzania.
millardayo.com : Siku unapigwa picha ukiwa na huyu mwanaume Club ulikua unajua unachukuliwa picha?
Kajala:
Siku hii ilikua ni birthday ya mwenye club, mimi sikujua kama napigwa
picha ndio zikasambazwa kwenye mtandao, wale wadada wamezichukua huko
ndio wakaanza kunitukana.
millardayo.com : Vipi kuhusu hii iliyoandikwa ya wewe
kukamatwa na dawa za kulevya Airport?
Kajala: Sio kweli manake hata dawa zenyewe za kulevya sijui zilivyo
zaidi ya kuziona tu kwenye TV, sasa hivi kila staa akipita kwenye uwanja
wa ndege Dar ni lazima asachiwe sana kwa sababu wanasema ‘nyinyi mastaa
mnatuharibia sana kazi’ kwa hiyo lazima wakuweke pembeni kukukagua.
millardayo.com : Safari yako ya China ilihusu nini?
Kajala: Nilikwenda kufanya shopping tu sababu ya movie yangu naanza
kushoot January 2014 kwa hiyo nikaenda kununua vitu vya kuvaa, sio
Camera wala vifaa… ni nguo tu, shopping inazidi milioni kumi.
millardayo.com Inaweza kutokea siku moja tukasikia Kajala kaolewa?
Kajala: Ndoa yangu ni ya kanisani ila sijui kama nitaruhusiwa kuolewa
tena kwahiyo namsubiria labda mume wangu akitoka Jela, sina mpango
wowote wa kuolewa kwa sasa japo napata usumbufu ila nawaambia tu mume
wangu yuko jela, huwa namtembelea kila weekend…. kukaa kwake jela
kumeniathiri sana, tulikaa kwenye ndoa miezi sita tu kabla ya misukosuko
kuanza, nilikua nampango wa kupata mtoto mwingine wa pili ili niwe
nimemaliza ila sasa hivi siwezi kuzaa, nimekaa tu namsubiria…..
credit to Millardayo.com