Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina
Maafisa
nchini Madagascar wanasema kuwa matokeo ya mwanzo mwanzo ya duru ya pili
ya uchaguzi wa Rais uliofanyika mwezi Disemba, yanaonyesha mshindi kuwa
waziri wa zamani wa fedha Hery Rajaonarimampianina.
Tume ya
uchaguzi ya nchi hiyo inasema kuwa bwana Hery Rajaonarimampianina
alishinda asilimia hamsini na tatu ya kura zilizopigwa.
Mshindani
wake, Jean Louis Robinson anasema kuwa uchaguzi ulikumbwa na wizi wa
kura na sasa anasema sharti shughuli ya kuhesabu kura irejelewe.
Uchaguzi huo ulikuwa mpango wa kurejesha utulivu kwa nchi hiyo baada ya mapinduzi ya kijeshi kufanyika miaka minne iliyopita.
Bwana
Rajaonarimampianina alikuwa mgombea aliyeungwa mkono na kiongozi wa
mapinduzi ya kijeshi, Rais wa zamani Andry Rajoelina.NA BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako