A

A

Hiki ndichokilichowatokea Waumini wale waliolishwa Nyasi,Ni hatari tupu


Waumini wa Mchungaji Daniel walijikuta wakianza kuumwa mara baada ya Mchungaji huyo kuwafanya wale wale majani.

Picha zinazofuata zinaonyesha watu tofauti wakiwa wagonjwa kwenye vyoo -  picha za vyooni zinawaonyesha wanawake wakishikilia matumbo yao, huku wanaume wakiwa wanatapika kwenye masinki.

Japokuwa Mchungaji huyo bado hajasema lolote juu ya tukio hilo ila kupitia ukurasa wake wa Facebook hapo jana aliandika: 'Mungu yupo kazini na watu wake wanatoa ushuhuda sasa'
Mchungaji Lesego Daniel
TAARIFA ZA KUIBUKA KWA KANISA HILO
Taarifa za kuibuka kwa kainsa hilo zilianza kusamba katika mitandao mbalimbali ya kijamii ambayo kwa nyakati tofauti iliripoti kuwepo kwa kanisa linaloimiza waumini wake kula nyasi kama ishara ya kutangaza miujiza ya Mungu.
Uchunguzi uliofanywa na Wadadisi wa Habari, ulibaini uwepo wa kanisa wa aina hiyo maeneo ya Upanga jijini Dar es salaam na huduma yao inafanywa kwa kutumia jina la Rabboni Centre Ministries yenye makao yake makuu jijini Pretoria, Afrika Kusini.
Waandishi wa Habari hizi, walifika Upanga, kwenye nyumba inayodaiwa kuwa ndilo kanisa hilo lakini hakuna mtu aliyekutwa hapo.

Hata hivyo, baadhi ya majirani walisema huwa wanawaona watu wakiingia katika nyumba hiyo lakini ajabu kunakuwa hakuna kelele zozote.

Chanzo chetu cha habari kimesema kuwa waumini wa kanisa hilo hula nyasi na baadaye kutapika, hali inayowafanya waamini kuwa kwa kufanya hivyo, wametakasika kiroho kwa kujazwa Roho Mtakatifu.
“Mchungaji wao huwakusanya waumini wake wanaopandisha mashetani wakiwa kanisani, hiyo hufanya shetani kumtoka mtu haraka,” kilisema chanzo.

Habari zinasema huduma hiyo ilianzishwa Afrika Kusini na Mtu anayejiita kuwa ni Mchungaji na Nabii Daniel Lesego mwaka 2002.

Imedaiwa kuwa kwa sasa waumini hao wapo kwenye mfungo ambao watu hufika kanisani na baadaye kula majani yaliyopo nje ya kanisa hilo wakisema kwamba Roho Mtakatifu huongoza mtu kula chochote huku ikidaiwa kuwa manyasi hayo ni chakula kutoka mbinguni.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako