A

A

Fahamu Kuhusu Msanii Mwana-FA kutoa Zawadi ya Gari kwa Meneja wa Ommy Dimpoz




MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya nchini, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’, amemzawadia gariaina ya Opha yenye thamani ya sh milioni 12, Meneja wa mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ommy Dimpoz, Mbarouk Issa ‘Mubenga’.
Zawadi hiyo ya FA imekuja baada ya meneja huyo kumsaidia baadhi ya
mambo ambayo yanahusika na muziki.
Akizungumza na
Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Mubenga alisema anamshukuru sana msanii huyo kwani hiyo imetokana na wao kuishi vizuri na kusaidiana katika kazi mbalimbali.

“Mimi namshukuru sana FA, na kinachotakiwa ni kushi kwa kusaidiana kati ya wasanii wenyewe na jamii nzima kwa ujumla, sidhani kama mimi ningekuwa na roho mbaya au FA angekuwa mmbaya kama ningepata zawadi hii, hivyo naomba tu tupendane,” alisema Mubenga.
Aliongeza kuwa upendo ni kitu kizuri hasa kwa watu ambao wanafanya kazi moja, hivyo ni vizuri kuwa na upendo kwa wote.
chanzo:tz daima