A

A

Exclusive: Dakika 4 na Hisia, Mshiriki wa TPF6. Mtazamo wake kwa TPF6, michongo aliyoipata na mipango yake 2014 (Audio)


Moja kati ya matukio ya kiburudani yaliyoteka attention ya wana Afrika Mashariki mwaka jana, ni shindano la kuimba la Tusker Project Fame 6 ambalo liliwakutanisha vijana wengi wenye uwezo mkubwa wa kuimba Afrika Mashariki.
Tanzania ilipeleka washiriki wanne (Angel, Tanah, Hisia na Durbat)  , ambapo Hisia pekee ndiye aliyepata nafasi ya kusimama kwenye jukwaa la fainali za shindano hilo akichuana vikali wa washiriki wenzake na mwisho kushika nafasi ya nne huku nafasi ya kwanza ikienda kwa Hope wa Burundi.
Tovuti ya Times Fm imepiga story na Hisia ili kufahamu machache ya muhimu kuhusu mtazamo wake kwa shindano la TPF6 na kipi anchodhani kilikuwa kikwazo kwake kuchukua ushindi huo pamoja na mipango yake binafsi katika kiwanda cha muziki wa Afrika Mashariki.
Haya ni Maoni yake baada ya kushindwa kuuchukua ushindi wa TPF6 pamoja na kuwa mshiriki ambaye hakuwa kikaangoni isipokuwa pale walipowekwa washiriki wote.
“Kwa maoni..Kura zilizidi, maana unajua kwa uwezo mwaka huu kila mtu aliyekuja kutoka nchi yake aliiwakilisha ipasavyo. Uwezo kila mtu alikuwa na uwezo na kila mtu alikuwa na kitu chake tofauti ambacho akienda stage watu wanabaki ‘jamaa anaweza hiki jamaa anaweza hiki’, kwa hiyo kila mtu alikuwa na uwezo na kila mtu alikuwa na nafasi.” Amesema Hisia.
Hisia amesisitiza kuwa kura ndizo hazikutosha, “ni kura, maana kinachoangaliwa mwisho wa siku ni kura. Ni mwenye kura nyingi ndiye anayeibuka kidedea, umeelewa.”
Mshiriki huyo ambaye tayari ameshaachia wimbo wake mpya alioupa jina la ‘Just for You’ ambao ulipokelewa vizuri zaidi kupitia mitandao mbalimbali, amesema anajiandaa kufanya wimbo mwingine na video ambavyo vitatoka rasmi mwezi wa kwanza mwishoni ama mwezi wa pili mwishoni.
Msikilize hapa kwa dakika takribani 4 akiongea na tovuti ya Times Fm:

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako