A

A

Dj Choka aeleza sababu za baadhi ya wasanii kukwepa kushiriki kwenye project zake, 'wengine huogopa kufunikwa'


Dj Choka ambaye anafanya kazi chini ya studio za B’Hitz ameelezea changamoto anazokutana nazo katika kufanya project zake zinazohusishwa collabo na wasanii mbalimbali wa hapa Tanzania na kutengeneza nyimbo kubwa zenye wakali kibao.

Akiongea  Dj Choka amesema kuwa anakutana na
changamoto kubwa katika kukamilisha project zake kwa kuwa wasanii wengine hukataa kujumuika katika wimbo aliouandaa kwa sababu tu wanaogopa kufunikwa na wasanii wengine ambao wamo kwenye hiyo project.

Amezitaja pia beef za chini chin kati ya wasanii huwafanya wasishiriki kwenye project hiyo pindi wanapogundua kuwa msanii flani ambaye hawapatani atakuwa kwenye wimbo huo.
“Unakuta labda wasanii wako tofauti kwa hiyo hawataki kuimba pamoja au labda wanaogopa mmoja atamfunika mwenzake. Yaani ni vibeef tu visivyo na msingi,  kwa hiyo hicho kinakuwa ni kikwazo kikubwa sana sasa inabidi uanze kuwachagua wasanii marafiki tu ndio mfanye nao kazi.” Dj Choka ameiambia tovuti ya Times Fm.

Ameongeza kuwa baadhi ya wasanii huchagua studio za kufanyia kazi,  “unakuta msanii unamwambia tunarekodi leo, anakuuliza ‘studio gani?’ Sasa unashindwa ufanyeje kwa kuwa na mimi hapa B’Hitz ndipo nipo label kwa hiyo kazi zote nafanyia hapa.”

Akielezea sababu zinazopelekea wasanii hao kuchagua studio ya kufanyia kazi, Dj Choka amesema wasanii wengine huwekewa masharti na studio zao wasifanye kazi katika studio nyingine lakini pia wengine huwa na mazoea ya kumtaka producer wanaemtaka wao na waliyezoea touch zake ndio wafanye nae kazi na sio yule aliyechaguliwa na yeye (mwenye wimbo).

Hivi karibuni Dj Choka aliachia wimbo wake ‘StingaLi’ na aliwashirikisha Dogo Janja aka Janjaro, Young Dee, Pluto, Country Boy, M-Rap Lion na Mis Rizzy.