Na Francis Godwin Blog
IKIWA
ni siku mbili toka katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya
Iringa Hassan Mtenga kumwagiza mstahiki meya wa Halmashauri ya
Manispaa ya Iringa Aman Mwamwindi kufuatilia kero mbili za wananchi
ikiwemo ya wagonjwa kukosa dawa katika Hospital ya mkoa na kujua fedha
za ruzuku ya jimbo la Iringa mjini ziko wapi na zinafanya nini,
mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa adai kuna kiasi
cha Tsh milioni 30 nyingine za mfuko wa jimbo.
Huku
mbunge Msigwa akiwaomba radhi wananchi wachache waliofika katika
mkutano huo kwa kudai kuwa haukutangazwa vya kutosha .
Hatua
ya katibu huyo kuagiza kufuatilia fedha hizo ni baada ya jimbo
hilo kukabiliwa na changamoto mbali mbali na fedha hizo zinazotolewa
na Rais zimelenga kusukuma maendeleo majimboni ila alihoji kwanini
Manispaa ya Iringa fedha zinakaa bila kazi.
Akizungumza
katika mkutano wake wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa
udiwani kata ya Nduli leo ,Msigwa alisema kiasi hicho cha Tsh 30m
zipo hadi sasa.
“Naomba
kuwahakikishieni nitaendelea kutafuta vyanzo vingine vya mapato
ili kusaidia kero za maji hapa Nduli ….mimi nasema ukweli namba mnipe
Ayub Mwenda nitafanya nae kazi”
Pia
Mbunge Msigwa amesema kuwa katibu wa CCM Hassan Mtenga si saizi yake
ila yeye saizi yake ni akina waziri mkuu Mizengo Pinda,waziri wan
chi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge na mbunge wa ISimani
Wiliam Lukuvi na katibu mkuu wa CCM Bw Kinana na sio yeye .
“Nataka
kuwahakikishia kuwa huyu mimi si saizi yangu saizi yake ni akina
Frank Nyalusi diwani wa Mvinjeni (Chadema) na katibu mwenzake wa
Chadema Iringa mjini Suazana Mgonakulima.
Wao
wanasema amekuja kwa ajili ya kunishughulikia mimi ila nasema njia
aliyojia atatitoka na njia hiyo hiyo kama walikuwepo akina Charles
Charles na wametoka zaidi ya makatibu 7 iwe yeye .
Hata
hivyo katika mkutano huo ambao idadi ya watu ilionekana ni ndogo
zaidi ukilinganisha na hali halisi ya nguvu ya Chadema
iliyokuwepo jimbo la Iringa mjini ,bado mbunge huyo alitumia
mkutano huo kuwaomba radhi wananchi kutokana na mahudhurio hayo hafifi
kwa madai haukutangazwa vya kutosha.
Kampeni
za uchaguzi mdogo wa kata hiyo ya Nduli zimeanza rasmi leo kwa
Chadema kufungua pazia hilo huku wao CCM wanataraji kuzindua
kampeni hizo katika eneo hilo la Nduli Januari 26 mwaka huu
Uchaguzi
huo mdogo umekuja kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo
Idd Rashid Chonanga aliyefariki duni kwa ugonjwa mapema mwaka jana.
Kwa
upande wake mgombea udiwani wa Chadema katika kata hiyo ya Nduli
Ayub Mwenda ambae alipata kuwa mwenyekiti wa kijiji cha Nduli kabla
ya CCM kumsimamisha nafasi hiyo kutokana na kuwa na tuhuma za
ubadhilifu wa fedha za maendeleo ,alisema kuwa yeye ana risiti za
fedha zote ambazo alikuwa akikusanya na kuwa kusimamishwa kwake nafasi
ya uenyekiti ni uoneu uliofanywa na aliyekuwa katibu wa CCM wilaya ya
Iringa mjini Lusiana Mbosa na kuwaomba wananchi kumkubali sasa ili
awe diwani wa kata hiyo.
Wachambuzi
wa masuala ya kisiasa mjini Iringa wanadai kuwa kipimo cha
kukubalika ama kutokukubalika kwa mbunge Msigwa katika jimbo hilo kwa
mwaka 2015 katika uchaguzi mkuu na mwaka huu katika chaguzi za
serikali za mitaa ni uchaguzi huo wa kata ya Nduli
|
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako