A

A

Baraza la Madiwani Kigamboni laridhia kugawanywa kwa jimbo hilo


MBUNGE wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile, amesema uamuzi wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Temeke kuridhia kuligawanya jimbo lake utakuwa na manufaa kwa maendeleo ya wakazi wake.

Alisema ukubwa wa Kigamboni yenye wakazi 750,000 na mahitaji yake kwa sasa inabidi mgawanyo huo ufanyike ili kusogeza maendeleo karibu, na kwamba wananchi wanapaswa kuunga mkono azimio hilo.

Dk. Ndugulile alitoa kauli hiyo jana alipozungumza na Tanzania Daima Jumapili ilipotaka kujua maoni yake kuhusu uamuzi huo wa Baraza la Madiwani wa Temeke ikiwamo kuwa na wilaya mpya.

Katika kikao cha baraza hilo lililokutana mwishoni mwa wiki, waliazimia kuanzisha wilaya ya Kigamboni, kutokana na maazimio hayo madiwani hao walipitisha mapendekezo ya kugawa kata za uchaguzi kutoka katika kata za Pemba Mnazi, Charambe na Mianzini, uamuzi uliokubaliwa kwa kauli moja na sasa unasubiri kuwasilishwa katika baraza la ushauri la mkoa kwa hatua zaidi.  --- via Tanzania Daima