Mshambuliaji
mpya wa Manchester United, aliyejiunga na wekundu hao akitokea Chelsea,
Juan Mata, akionyesha Jezi yake namba 8, aliyokabidhiwa mara baada ya
kumwaga wino katika chama lake jipya hilo.
**********************************
*MOYES AANZA KUCHONGA NGENGA
Siku
chache tu baada ya kumnasa mshambuaji hatari, Kocha wa Manchester
United, David Moyes sasa ameanza kuchonga na kujigamba kuwa anauhakika
wa kurudisha matumaini kwa timu yake katika mechi zake zilizobaki baada
ya kumsajiri mshambulizi huyo kwa dau la Pauni milioni 37 ambazo ni
zaidi ya Sh. bilioni 70 za kitanzania.
Aidha
Moyes aliongeza kwa kusema kuwa anatarajia kuendelea kufanya usajiri
mkubwa na wa nguvu, siku zijazo kwa lengo la kuijenga timu itakayokuwa
ya ushindani.
''Sitarajii
kusajiri mchezaji mwingine katika kipindi hiki cha dirisha dogo bali
najiandaa kukiimarisha kikosi changu nilichonacho kwanza,
Kwa ujio wa Mata kwangu ni faraja kubwa kwa kujiunga katika wakati huu muafaka''. alisema Moyes

No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako