Muda mfupi kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo, asubuhi
kulitokea fujo baada ya jamaa mmoja alieshtukiwa kwamba anarekodi
mazungumzo ya moja kati ya vikundi vilivyokua vimesimama kwenye kordo ya
Mahakama kuanza kushambuliwa.
Yani ilikua hivi…….. wakati kesi inasubiriwa kuanza kusikilizwa
kulikua na makundi mbalimbali ya hawa Wafuasi, wengine upande wa
Chadema, wengine upande wa Mbunge Zitto Kabwe ambapo kwenye hivyo
vikundi ndio kuna kimoja kikaanzisha vurumai baada kushtukia mchezo.
Mpaka mwisho, hakikujulikana kilikua kikundi cha upande gani kati ya
hizi pande mbili za hii kesi ambayo imeahirishwa mpaka Jumatatu January 6
2014.
Credit;millardayo
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako