MWANAMKE anayefahamika kwa jina la mama Eric, hivi karibuni muda wa saa 11 jioni alijikuta akijifungua mtoto wa kiume Barabara ya Posta jijini hapa kufuatia kushikwa na
uchungu ghafla.
Akina mama waliomsaidia mama Eric kujifungua wakiwa na mtoto aliyezaliwa.
Akiwa katika hali ya kuhangaika kusukuma mtoto, mwanamke huyo aliishiwa nguvu huku tayari kichwa cha mtoto kikiwa kimetokeza nje, ndipo mama mmoja aliyekuwa akisafiri akajitokeza kumsaidia kumzalisha.
“Nilimwona akihangaika kusukuma mtoto, lakini akaishiwa nguvu. Nilimwonea huruma nikatua begi na mkoba, nikamshika mikono akaja mama mwingine tukasaidiana kumzalisha,” alisema mama huyo aliyejitambulisha kwa jina la Euphrazia John, mkazi wa Bariadi, Simiyu.
Euphrazia alisaidiana na akina mama wengine, Juliana Wambura na mke wa diwani wa zamani wa Kata ya Nyamagana, Mama Mkiwa.
Baadaye wanawake hao walimpeleka mzazi huyo nyumbani kwao Capri Point jijini hapa.
Mama Eric akiwa kwenye gari kuelekea nyumbani.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako