Joy na Maurus wakiwaongoza watanzania kuimba wimbo wa Taifa.
Mhe. Balozi Tuvako Manongi akizungumza machache.
Sehemu ya Wageni
Mhe. Balozi Tuvako Manongi akikata keki wengine
onesho la mavazi yaliyobeba maudhui ya utamaduni wa mtanzania yalitia fora sana
picha ya kuchora
Watanzania wakiserebuka.
Jumuiya
ya Watanzania Jijini New York na Vitongoaji vyake jana Jumamosi
imesherehekea miaka 52 ya Uhuru wa Tanganyika, katika Hafla iliyojaa
nderemo, shamrashamra zikiambatana na muziki, chakula, vinywaji na
maonyesho ya nguo zilizokuwa na maudhui ya utamaduni na desturi ya
mtanzania. Sherehe hizo zilitanguliwa na mchezo wa mpira wa miguu kati
ya Timu ya New York na Timu ya ....... ambako timu ya New York
iliibuka kidedea.
Mgeni
Rasmi katika sherehe hizo zilifana kiaina yake alikuwa ni
Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Katika Umoja wa Mataifa, Balozit
Tuvako Manongi ambaye alifuatana na Naibu wake Balozi Ramadhan Mwinyi
na tukaungwa mkono na Balozi wa Somalia katika Umoja wa Mataifa .
Watanzania hawa alisimama kwa sekunde Moja, kumukumbuka na kumwombea
Marehemu Rais wa Kwanza wa Afrika ya Kusini Huru, Mzee wetu Nelson
Mandera.
katika
Salamu zake fupi alizozitoa kwa watanzania hao wa Jiji la New York
na Vitongoji vyake, pamoja na kuishukuru Jumuia hiyo ya Watanzania kwa
maandalizi mazuri ya sherehe hizo, Balozi Tuvako Manongi amewaasa
watanzania hao kuendeleza na kujenga misingi ya utaifa, uzalengo,
kupendana na kuheshimiana.
Akasema
kila mtanzania anayohaki ya kuwa mfuasi wa chama chochote kile cha
siasa, lakini jambo kubwa na la msingi linalowaunganisha watanzania
popote pale walipo si itiakadi za vyama bali ni utanzania wao ambao
umejengekea katika misingi ya utaifa, uzalendo, kuheshimiana, kupendana
, kusaidiana ikiwa ni pamoja na kuitetea nchi yao.
Kwa
upande wao, Jumuiya hiyo ya Watanzania katika Salamu zao kwa
Serikali kupitia Balozi Manongi, wameomba suala la uraia wa nchi
mbili lipewe umuhimu wa pekee katika mwenendo mzima wa mchakato wa
Katiba mpya unaoendelea.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako