Afisa
Habari kutoka Kitengo cha Habari Umoja wa Mataifa(UNIC), Usia Nkhoma
Ledama akizungumza leo jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari
katika hoteli ya Holiday Inn juu ya changamoto na mafanikio ya mkutano
wa mwisho wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 19) na msimamo wa Tanzania na
Bara la Afrika kwa ujumla juu ya masuala ya Tabianchi na Mazingira
duniani. Kutoka kulia ni Mtaalamu wa mambo ya Nishati na Mabadiliko
ya Tabianchi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bw.
Abbas Kitogo, Mwakilishi kutoka Youth of United Nations Association
(YUNA) Adam Anthony na mgeni rasmi Naibu Mkurugenzi Msaidizi wa kitengo
cha Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi.
Naibu Mkurugenzi
Msaidizi wa kitengo cha Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard
Muyungi akizungumza na waandishi wa habari juu ya mkutano wa mabadiliko
ya Tabianchi (COP 19) amesema kuna ugumu na
umuhimu wa mkutano wa mabadiliko ya Tabianchi, na kuongeza kuwa
wamekubaliana wawe na mkataba kwa nchi wanachama jinsi ya kupunguza
uzalishaji wa hewa ukaa kwa kiwango ambacho hakitaongeza Madini Joto
duniani
Muyungi
alisisitiza kwamba kuna umuhimu wa wanachama kukubaliana kwa maandishi
na kuandika mkataba vile vile amesema walikubaliana kutokufuta mkataba
mama wa 1992, na umuhimu wa kupunguza Gesi Joto na kuangalia uchangiaji
wa tatizo la Madini Joto katika duniani.
Mtaalamu
wa mambo ya Nishati na Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bw. Abbas Kitogo, akizungumzia
masuala ya mipango ya serikali kuhusu mabadiliko ya Tabianchi kupewa
kipaumbele katika mipango ya serikali kwa maendeleo ya Taifa kwa
kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, alisisitiza
kwamba UNDP ina nafasi ya kusaidia kuleta maendeleo kwa Taifa kwa kuweka
mipango ya maendeleo yenye kuendana na mabadiliko ya Tabianchi.
Bw.
Anthony amefafanua kuwa baada ya mkutano wa COP 19 uliofanyika Warsaw
Poland, hivi karibuni kujipanga kwa vijana na vyombo vya habari katika
na mkutano unaokuja wa 2015 wa mabadiliko ya Tabianchi.
Fazal
Issa kutoka Mtandao wa Asasi Zisizo za Kiserikali zinazofanya shughuli
zake katika Masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi akizungumza kwa undani
matokeo ya mabadiliko ya Tabianchi kwa nchi masikini na jinsi
zinavyoweza kurudisha nyuma maendelo ya sehemu husika.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa kufafanua yaliojiri
katiak mkutano wa Warsaw, Poland wa Mabadiliko ya Tabianchi.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako