Wapinzani wakijaribu kuvamia ofisi ya waziri mkuu.
Mabomu ya machozi yakiwa yamepigwa katika mitaa ya Bangkok.
Maji yakimwagwa kuwazuia waandamanaji.
Mabomu ya machozi yakiwa yamepigwa katika mitaa ya Bangkok.
Maji yakimwagwa kuwazuia waandamanaji.
Vikosi vya tiba vikiwasaidia waliojeruhiwa katika maandamano.
WAZIRI Mkuu wa Thailand, Yingluck Shinawatra, amekataa madai ya
waandamanaji wanaomtaka ajiuzulu akisema hilo haliwezekani chini ya
katiba ya sasa nchini humo, lakini akasema yuko tayari kwa mazungumzo.
Maandamano makubwa leo yalifanywa na wananchi ambapo walijaribu
kuivamia ofisi ya waziri mkuu huyo katika mapambano ambayo tangu yaanze
watu wane wamekufa katika machafuko hayo ya kisiasa.
Waandamanaji wanaoipinga serikali wamemtaka Bi Yingluck kujiuzulu,
ambapo mpinzani wake, Suthep Thaugsuban, amempa siku mbili kufanya
hivyo. Waandamanaji wanataka serikali ichukuliwa na “Baraza la Umma”
wakidai serikali ya Yingluck inaongozwa na kaka yake ambaye aliangushwa,
Thaksin Shinawatra.
CHANZO BBC NEWS
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako