Muwakilishi
wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi,
akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya mwaka 2013 ambayo hutolewa
kila mwaka na Shirika la Afya Duniani, Balozi aliwaeleza wageni
waalikwa katika hafla hiyo kwamba ushiriki wa viongozi wa afrika kupitia
mtandao wao wa ALMA umechangia sana katika kupunguza idadi ya vifo
vitokanavyo na Malaria
Dkt.
Robert Newman kutoka WHO yeye amesema, inasikitisha pale inapobidi
mtoto apoteze maisha kwa sababu tu ameshindwa kupatiwa chandarua
ambayo thamani yake ni dola tano. amewataka viongozi na washirika
mbalimbali kutobweteka na mafanikio katika kuudhibiti ugonjwa huo
mafanikio nayohusu kupungua kwa maambukizo ya ugonjwa wa malaria na vifo
vya watoto chini ya miaka mitano
Dkt. Fatoumata Traore ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa Roll Back Maralia akizungumza wakati wa halfa hiyo
Katibu Mtendaji wa ALMA Bi. Joy Phumapi naye akizungumza machache
Bw,
Ray Chambers ambaye ni Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, amesema inatia moyo sana kuona vitanda katika wadi za watoto
vikiwa vitupu mahali ambapo watoto walikuwa wakilala wawili katika
kitanda kimoja kutokana na kusumbuliwa na malaria.
Na Mwandishi
Maalum
Utashi wa kisiasa
unaoonyeshwa na marais wa Afrika katika kudhibiti ugonjwa wa malaria, pamoja
na ushiriki wa wadau mbalimbali akiwamo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon
umeanza kuzaa matunda kufuatia
taarifa za kutia matumaini zinazoonyesha kupungua kwa vifo vitokanavyo na ugonjwa wa
malaria
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya mwaka 2013 ya Shirika la
Afya la Dunia ( WHO ) kuhusu mwelekeo wa ugonjwa wa malaria katika kipindi hicho , Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania
katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako
Manongi amesema hapana shaka kwamba mwamko
ulioonyeshwa na Marais wa Afrika kupitia muungano wao dhidi ya Malaria ( ALMA) umechangia kwa kiasi kikubwa.
Jana
Alhamis Bw. Ray Chambers ambaye
ni mjumbe maalum wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Malaria kwa pamoja
na Dkt. Robert Newman ambaye ni Mkurugenzi wa mradi wa Malaria (WHO),
Bi. Fatoumata Traore Mkurugenzi Mtendaji
wa Roll Back Malaria na Bi. Joy Phumapi
ambaye ni Katibu Mtendaji wa ALMA walizindua
ripoti hiyo mbele ya Wawakilishi
wa Kudumu wa Nchi za Afrika na wadau wadau wengine.
Akiwakaribisha wageni waalikwa kwa niaba ya Balozi wa Msumbiji katika hafla
hiyo iliyoandaliwa na ALMA, Balozi Manongi alisema ripoti za kila mwaka za WHO zimekuwa
zikionyesha mwelekeo mzuri katika
kuushughulikia ugonjwa huo ambao
unaadhiri kwa kiasi kikubwa watoto wadogo chini ya umri wa miaka mitano.
Na kusisitiza kwamba Afrika inatakiwa kuzitumia ripoti hizo kuongeza kasi
katika kuikabili Malaria.
“Ripoti hizi zinaonyesha kwamba tukishirikiana
tunaweza kabisa kuidhibiti malaria, viongozi wetu wameonyesha mfano kwa
kuanzisha muungano wao dhidi ya malaria,
ni wajibu wetu kuendelea kukusanya nguvu na kujituma Zaidi ili tusirudi nyuma”
akasisitiza Balozi Manongi.
Ripoti
ya malaria kwa mwaka huu, ambayo ni
mkusanyiko wa taarifa kutoka nchi 102 zikiwamo 10 ambazo zimeathirika
sana na ugonjwa wa
malaria na taarifa kutoka vyanzo vingine, inatoa tathmini ambayo
pamoja na mambo mengi kwamba onyesha ushirikiano kati ya serikali,
mashirika ya
kimataifa na wafadhili umewezesha katika kipindi cha mwaka 2000-2012
kuokoa
maisha ya watu 3.3 milioni ambayo yangepotea kutoka na ugonjwa
huo.
Taarifa hiyo inaeleza Zaidi kwamba ugonjwa wa malaria umepungua kwa asilimia 45 duniani kote na kwa asilimia 49 katika nchi
za Afrika zinazohudumiwa na WHO.
Akizungumza
katika uzinduzi huo Dkt. Robert Newman kutoka WHO amewaeleza
Mabalozi kwamba ripoti inahabari njema kuwa ugonjwa wa malaria
umepungua kwa kiasi kikubwa sana katika kipindi hicho cha kati ya
2000-2012
“ kuna punguzo la asilimia 54 la vifo vya watoto
wadogo chini ya umri wa miaka mitano vitokanavyo na malaria katika nchi za
afrika hususani zile ambazo zimeathirika
Zaidi. Takwimu hizi na nyingine zilizomo
katika ripoti hii zinathihirisha wazi
kwamba tukishirikiana tunaweza kuleta
mabadiliko makubwa katika kuikabili Malaria” akasema Dkt Newman
Akaongeza kwamba licha
utashi wa kisiasa ulioonyeshwa na viongozi mbalimbali kumekuwapo na mwitikio
unaoridhisha wa uchangiaji wa raslimali fedha katika eneo hilo. Ambapo katika
kipindi hicho jumla ya dola za kimarekani bilioni mbili zilitolewa na
wafadhili na dola milioni mia
tano zilitolewa na nchi ambazo
zimeathirika Zaidi.
Hata hivyo akasema ingawa mwamko wa kuchangia umekuwa mkubwa bado lengo halijafikiwa la kiasi cha dola za
kimarekani 5.1 na kuonya kwamba bado
michango inahitaji na wala mafanikio hayo yaliyopatikana
yasijewafanya wadau wakabweteka kuchangia au kuhamishia fedha kwenye masuala mengine.
“ hatupashwi kubweteka au kuridhika na mafanikio
haya, haipendezi mtoto au mtu kufariki kwa sababu tu ya kushindwa kuwa na
uwezo wa kununua chandarua ambayo
thamani yake ni sawa na dola tano ya kimarekani. Na weza kusema
mafaniko haya ni sawa na nusu glasi. Hebu pata picha kama wewe ungekuwa ni mtoto
unayeishi katika maeneo ambayo yameathirika vibaya na malaria halafu hakuna
hata dawa za kukutibu, bila shaka matarajio yako ni kuona glasi imejaa na
si nusu glasi au glasi iliyotupu” akasisitiza Muwakilishi huyo wa WHO.
Naye Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu Malaria na ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuchagiza na
kutafuta raslimali zikiwamo fedha
kwaajili ya miradi ya malaria, Bw. Ray Chambers alikuwa na haya ya kusema
“Ripoti hii ya
WHO inatoa matumaini sana, ukizingatia
kwamba katika miaka iliyopita takribani
watoto milioni moja walikuwa wakipoteza maisha kwa malaria leo hii idadi hiyo imepungua hadi
kufika nusu ni jambo la kutia faraja
sana” akasema Chembers
Na kuongeza. “ nimetumia muda mwingi Afrika nimeshuhudia watoto wakifariki, nimejionea wadi za watoto zilivyokuwa zimejaa huku watoto wakilala wawili katika kitanda kimoja. Lakini leo hii katika baadhi ya nchi wadi za watoto zipo tupu na vitanda vinatumika kwa huduma nyingine”.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako