Mshehereshaji Bw. Salum Msellem kutoka Istiqama Radio akitambulisha
meza kuu kwa washiriki wa mafunzo ya Ujasiriamali ya siku moja kwa
Vijana Visiwani Pemba yaliyofanyika mwishoni mwa juma kwenye ukumbi wa
Shule ya Sekondari Madungu.
Mratibu wa YUNA kisiwani Pemba, Bw. Mohammed Ali, akisoma taarifa ya
maendeleo ya vilabu vya Umoja wa Mataifa visiwani humo na changamoto
zinazowakabili kwa walezi wa vilabu hivyo.
Afisa Vijana - Mshauri kutoka WIZARA ya Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya
Vijana, Wanawake na Watoto, Bi. Stara Salim akizungumzia jitihadi za
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuwawezesha Vijana kupata mikopo
kupitia asasi mbalimbali za fedha ili waweze kujikwamua kimaisha na
kuondokana na lindi la umaskini visiwani Pemba.
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia
Nkhoma Ledama akizungumzia lengo la kuendesha mafunzo ya Ujasiriamali
kwa watu walio nje ya shule ikiwa ni moja ya agenda ya kutekeleza
malengo ya milenia ya kupunguza umaskini kwa nchi zinazoendelea.
Mkufunzi wa mafunzo ya Ujasiriamali kupitia Program ya kazi Nje nje
inayolenga kuelemisha Vijana stadi za Ujasiriamali iliyoasisiwa na
Shirika la Kazi Duniani (ILO) Bi. Mwanapili Hamad akitoa mada kuhusu
dhana nzima ya uongozi katika biashara (Business Management) kwa
wajasiriamali Vijana visiwani Pemba ili waweze kuboresha kipato chao.
Picha juu na chini ni sehemu ya washiriki wa mafunzo ya Ujasiriamali ya
siku moja yaliyoratibiwa na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa
(UNIC).
Mjasiriamali mwenye kipaji cha kuchora ramani za majengo, kutengeneza
sampuli za nyumba kwa kutumia maboksi Bw.Steven Timothy Mihale kutoka
Temeke Youth Development Network (TEYODEN) akionyesha moja ya kazi zake
kwa wajasiriamali wenzake ambayo inampatia kipato na kuweza kuendesha
maisha yake.
Bw. Steven Mihale aliwapa moyo wajasiriamali wenzake na kuwataka kuwa na uthubutu na kutokata tamaa mapema.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo akiuliza swali kwa wakufunzi wa
mafunzo ya Ujasiriamali yaliyoratibiwa na Kituo cha Habari cha Umoja wa
Mataifa (UNIC).
Mkufunzi wa mafunzo ya Ujasiriamali Bi. Mgeni Salum akitoa somo la
namna ya kuhifadhi hesabu za mauzo na kujua kama biashara ina faida au
hasara sanjari na kupata mikopo kupitia taasisi za kifedha.
Mratibu wa YUNA kisiwani Pemba, Bw. Mohammed Ali akiteta jambo Mkutubi
wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Harriet Macha
(katikati) wakati wa mafunzo ya Ujasiriamali kwa vijana visiwani Pemba
yaliyofanyika kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari Madungu.
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia
Nkhoma Ledama, akifunga mafunzo ya siku moja ya wajasiriamali Visiwani
Pemba yaliyoratibiwa na kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC).
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako