Joseph Kahama aahidi ushirikiano na wachimbaji wadogo nchini; Asema sekta ya madini kuongeza mchango wake kwenye pato la Taifa
Habari na Damas Makangale, MOblog — Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini nchini (Tanzania Chamber of Minerals and Energy) Joseph Kahama amesema chama kwa kushirikiana na chuo cha Ufundi Veta Moshi wataendelea kupeleka vijana wazawa wa kitanzania kwenda kupata mafunzo ya mambo ya uchimbaji na utafutaji wa Madini (Geology).
Akizungumza na MOblog jana kwenye mahojiano maalum baada ya kumaliza mkutano wao wa mwaka kwa wanachama wake, Joseph Kahama amesema chama chao kwa kushirikiana na serikali wataendelea kusaidia vijana wa Kitanzania kupata

elimu ya kutosha katika sekta ya madini nchini: “Tumeshapeleka vijana
kadhaa kwenye mafunzo mahsusi ya madini na wengi wao wameshapata kazi
katika kampuni kadhaa za madini hapa Tanzania,” amesema.
Kahama alisisitiza kwamba si kweli kwa wageni wengi ndio wameajiriwa katika sekta madini kuliko wazawa kwa sababu kwa takwimu asilimia 90 walioajiriwa sasa katika migoi mbalimbali ni watanzania.
Alisisitiza kwamba wataendelea na mkakati wao wa kuwajengea uwezo wa sawa (skills)katika uchimbaji na utafutaji wa madini ili kuongeza ajira kwa vijana na kutokomeza umaskini hapa nchini.
Amesema kwa sasa wana malengo kwa kushirikiana na serikali kuangalia kwa jinsi gani wanasema kuongeza mchango wa sekta ya madini katika pato la taifa kutoka 3.7 asilimia mpaka asilimia 10.
Kahama amesema kwamba kwa kushirikiana na serikali wataendelea kusukuma gurudumu la maendeleo kupitia sekta ya madini na kuhakikisha kwamba wazawa wananufaika vya kutosha kutokana na mchango wa sekta hiyo kwenye uchumi wa taifa.
Amesema pia wadau katika sekta hiyo wanawakaribisha wachimbaji wadogo wadogo wawe wanachama wa chama chao ili waweze kusaidiana na kukabiliana na changmoto mbalimbali.
Kahama aliahidi kwamba wanachama na wachimbaji wote wa madini watashirikiana katika kuweka mazingira safi wakati wote wa utafutaji na uchimbaji wa madini katika maeneo husika.

Mgeni Rasmi katika sherehe za mwaka za Chama cha Wafanyabiashara wa
Madini Tanzania (Tanzania Chamber of Minerals and Energy) Katibu Mkuu
Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi akizugumza kwa niaba ya Waziri
kwa wageni waalikwa na mabalozi.(Picha na Zainul Mzige)
Mwenyekiti wa Tanzania Chamber of Minerals and Energy, Joseph Kahama
akizungumza wakati wa sherehe hizo jana usiki katika hoteli ya Golden
Tulip jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo Mabalozi wakifuatilia tukio hilo.
Wadau wa sekta ya madini nchini wakibadilishana mawazo kwenye Gala
Dinner party ya wadau wa Sekta ya madini na Serikali iliyofanyika kwenye
Golden Tulip jijini Dar.
Mgeni Rasmi katika sherehe za mwaka za Chama cha Wafanyabiashara wa
Madini Tanzania (Tanzania Chamber of Minerals and Energy) Katibu Mkuu
Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi akiongozana na Mwenyekiti wa
Tanzania Chamber of Minerals and Energy, Joseph Kahama kwenye meza ya
chakula wakati wa halfa ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Chama cha
Wafanyabiashara wa Madini Tanzania.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Mwenyekiti wa Tanzania
Chamber of Minerals and Energy wakiongoza wageni waalikwa kupakua
chakula.
Wageni waalikwa wakijisevia chakula cha usiku.
Mwenyekiti wa Tanzania Chamber of Minerals and Energy, Joseph Kahama akibadilishana mawazo na wageni waalikwa.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi akisalimiana na
Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Ryan Bert and Compay Limited na
Swordfish Security Consultants Haki Ngowi liyeambatana na mdogo wake
mbunifu wa mavazi nchini Sheria Ngowi.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi akifurahi jambo na baadhi ya wageni waalikwa.
Mwenyekiti wa Tanzania Chamber of Minerals and Energy, Joseph Kahama
akibadilishana mawazo na baadhi ya wadau wa sekta ya madini. Kushoto ni
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi na Wa pili kushoto
Katibu Mkuu wa Tanzania Chamber of Minerals and Energy, Bw Emmanuel
Jengo.
Makamu wa rais wa Africa Barrick Gold Bw. Deo Mwanyika (wa pili
kushoto) akibadilishana mawazo na Waheshimiwa mabalozi kwenye Gala
Dinner Party iliyoandaliwa na Tanzania Chamber of Minerals and Energy
kwenye hoteli ya Golden Tulip.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Bw. Eliakim Maswi akiteta jambo na Mmoja wa wadau katika sekta ya Madini.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako