Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Rasimu ya pili ya Katiba Mpya kutoka
kwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba wakati wa
hafla ya kukabidhiwa rasimu hiyo iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya
Karimjee jijini Dar es Salaam.Rais Kikwete aliitaka Tume hiyo ya Katiba
kuhakikisha kuwa Rasimu hiyo inawekwa kwenye mitandao yote ya kijamii
ili wananchi waweze kuisoma na kuielewa na kuweza kutoa maoni yao kwa
urahisi kupitia mitandaoni.
Rais
wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akipokea Rasimu ya pili ya Katiba
Mpya kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba
wakati wa hafla ya kukabidhiwa rasimu hiyo iliyofanyika leo kwenye
Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rasimu hiyo kwa Makamu wa
Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal mara tu baada ya kukabidhiwa na
Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rasimu hiyo kwa Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rasimu hiyo kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Maalim Seif Shareef Hamad.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rasimu hiyo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rasimu hiyo Rais Mstaafu wa awamu ya Pili,Mzee Ali Hasaan Mwinyi.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rasimu hiyo kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mzee Cleopa Msuya.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar,Mh. Pandu akipokea Rasimu hiyo.
Spika wa Bunge.
Jaji Mkuu.
Jaji Mkuu wa Zanzibar.
Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue.
credit: Michuzi-matukio blog
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein na Makamu
wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali wakiwapongeza wajumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya katiba baada ya makabidhiano ya Rasimu ya pili ya Katika
katika viwanja vya Karimjee Hall jijini Dar es salaam
Picha ya pamoja na wajumbe wa tume
Rais
Kikwete akizungumza na Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahim Lipumba na wa
NCCR Mageuzi Mhe James Mbatia mara baada ya kukabidhiwa na Rasimu ya
katiba mapema leo,ambapo hafla hiyo imefanyika viwanja vya Karimjee
jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa,Wanasiasa na
Wanaharakati,Shoto ni Waziri mkuu Mstaafu,ambaye pia ndiye Mwenyekiti
wa Tume ya Mabadiliko ya katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba
akishuhudia.PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako