· KUFUATIA
TUKIO LA MAUAJI LILITOKEA MNAMO TAREHE 19.12.2013 MAJIRA YA SAA
14:00HRS HUKO KATIKA ENEO LA TAZARA -TUNDUMA KATA NA TARAFA YA
TUNDUMA WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA. AMBAPO MTOTO KALIBU S/O
KIMWELU, MIAKA 6, MNYAMWANGA, MKAZI WA MTAA WA TAZARA TUNDUMA ALIUAWA
KWA KUCHINJWA SHINGONI KWA KUTUMIA KISU NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.
AIDHA WATU HAO WALIMNYONGA SISTA D/O NYILENDA, MIAKA 17, MNYIHA,
MFANYAKAZI WA NDANI [HOUSE GIRL] KWA KUTUMIA WAYA WA TELEVISHENI
ULIOKUWEPO SEBULENI. MBINU NI KUWAVAMIA WAHANGA WAKIWA NDANI NYUMBANI
KISHA KUWAUA KINYAMA. MIILI YA MAREHEMU WOTE ILIKUTWA SEBULENI. WAKATI
WA TUKIO BABA WA MTOTO AITWAE ESTON S/O KIMWELU,MIAKA 55, MNYAMWANGA,
DIWANI WA KATA YA MKANGAMO – CCM, MKAZI WA TAZARA ALIKUWA SHAMBANI
KIJIJI CHA KIPAKA NA MAMA WA MTOTO AITWAE TUMAINI D/O YOHANA, MIAKA 29,
MNDALI, KATIBU MUHTASI HALMASHAURI YA MJI MDOGO WA TUNDUMA ALIKUWA
KAZINI. KATIKA TUKIO HILO WATU HAO PIA WALIIBA MABEGI MAKUBWA MAWILI
YENYE NGUO MBALIMBALI YALIYOKUWA KATIKA CHUMBA WANACHOLALA WATOTO.
· KATIKA
TUKIO HILO MMOJA WA WATILIWA MASHAKA WALIOKUWA WAMESHIKIWA NA JESHI LA
POLISI KWA MAHOJIANO NA UCHUNGUZI ZAIDI AMBAYE NI NDUGU WA MAREHEMU
ENOCK S/O SIMWELU, MIAKA 23, MNYAMWANGA, MKULIMA AMEKIRI KUHUSIKA NA
TUKIO HILO AKISHIRIKIANA NA GABRIEL S/O KIMWELU, MIAKA 19, MNYAMWANGA,
MKULIMA. WOTE NI WATOTO WA MKE MKUBWA, WAKAZI WA MAJENGO MAPYA TUNDUMA
NA PATRICK S/O MSIGWA, MIAKA 18, MKINGA, MKULIMA MKAZI WA MAJENGO MAPYA
TUNDUMA NI MAJIRANI NA RAFIKI WA WATOTO HAO.
· AIDHA
AMESEMA KUWA CHANZO CHA KUHUSIKA NA MAUAJI HAYO NI KUTOKANA NA BABA YAO
KUWATELEKEZA NA KUANDIKA MALI ZAKE ZOTE KWA JINA LA MAREHEMU KALIBU S/O
KIMWELU KUWA MRITHI WA MALI HIZO.
· KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL
MASAKI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUZINGATIA SUALA LA MALEZI BORA KWA
WATOTO NA VIJANA WAO ILI WAKUE KATIKA MAADILI MEMA NA KUJIEPUSHA NA
MATUKIO YA UHALIFU.
{B.N.MASAKI — ACP )KAIMU: KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako