Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu TFF
|
MECHI YA MTANI JEMBE YAINGIZA MIL 422/-
Mechi
ya Nani Mtani Jembe kati ya Yanga na Simba iliyochezwa juzi (Desemba 21
mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Simba kuibuka na ushindi wa
mabao 3-1 imeingiza sh. 422,611,000.
Mapato
hayo ni kutokana na washabiki 52,589 waliokata tiketi kushuhudia mechi
hiyo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh.
20,000 na sh. 40,000. Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia
watazamaji wengi ambapo walikuwa 19,044.
Asilimia
18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa kutokana na mapato
hayo ni sh. 64,466,084.75 wakati gharama za kuchapa tiketi ni sh.
7,488,000.
Mgawo
mwingine ilikuwa kama ifuatavyo; kila klabu imepata sh. 117,470,066.61,
asilimia 15 ya uwanja ni sh. 52,598,537.29, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira
wa Miguu (FDF) sh. 35,065,691.53 wakati gharama za mchezo zilikuwa sh.
28,052,553.22.
MALINZI, MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa na
mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika kesho (Desemba 24 mwaka
huu).
Mkutano huo utafanyika saa 6 kamili mchana kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako