A

A

RONALDO" NIPO FITI KABISA KUREJEA UWANJANI "

MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo amepona maumivu ya misuli na yuko tayari kurejea uwanjani, amesema nyota huyo wa Real Madrid na Ureno leo. Ronaldo aliumia nyama za paja akiichezea Real mechi ya La Liga dhidi ya Almeria Novemba 23 na akakosa mechi ya Ligi ya Mabingwa timu yake ikishinda dhidi ya Galatasaray na Jumamosi katika La Liga Real ikiifunga Valladolid.
Niko fiti; Ronaldo amesema atarejea uwanjani katika mchezo ujao wa Real
“Sina tena majeruhi,” amesema Ronaldo katika sherehe za tuzo mjini Madrid. “Nimekuwa vizuri kwa siku kadhaa sasa,”aliongeza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ambaye amekuwa vizuri mno msimu huu. “Tuliona bora kutolazimisha mambo katika mechi na Valladolid, lakini nitakuwepo katika mchezo ujao kwa uhakika,”.Ronaldo amefunga mabao 14 katika mechi zake saba zilizopita za klabu nan chi yake kabla ya kuumia nan i miongoni mwa wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia ya FIFA, Ballon d'Or mwezi ujao. Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United alikuwa wa mwisho kushinda tuzo hiyo mwaka 2008, kabla ya mshambuliaji wa Barcelona na Argentina, Lionel Messi kushinda mara nne mfululizo tuzo zilizofuiata. Mechi ijayo ya Real ni ya Kombe la Mfalme hatua ya 32 bora, mechi ya kwanza dhidi ya timu ya Daraja la Pili,  Olimpic de Xativa Jumamosi na watacheza na FC Copenhagen katika Ligi ya Mabingwa Jumanne ijayo. Mabingwa hao maea tisa Ulaya tayari wamefuzu hatua ya 16 bora kama vinara wa Kundi B.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako