A

A

Rais Obama amkumbuka Mandela kwa sifa tele akimtaja kama kielelezo cha mabadiliko na mkongwe wa historia asiye na mfano

Obama waves as he arrives to speak to crowds attending the memorial service for former South African president Nelson Mandela at the FNB Stadium in Soweto near Johannesburg
Rais wa Marekani Barack Obama leo Jumanne ameungana na Waafrika Kusini katika kumkumbuka rais wa zamani wa taifa hilo Nelson Mandela ambapo amemsifia na kumtaja kama mkongwe wa historia ambaye amepata nafasi hiyo katika vizazi kupitia mapambano, msimamo imara katika maamuzi, na kwa kuonyesha uwezo katika maamuzi ya kisiasa.
Obama amemtaja Mandela kama kielelezo cha jinsi gani watu wanaweza kufikia mabadiliko kwa kupigana kwa ajili ya maadili yao na kujenga hoja na sababu kufikia kujitoa kwao.
Obama amesema kuwa ni vigumu kumsifia mtu yeyote , lakini ni vigumu zaidi kufanya hivyo hasa kwa mkongwe wa historia , ambaye amelifikisha taifa katika haki,na mtu aliyemfanya yeye ashawishike kuingia katika siasa, Nelson Mandela.
Aidha rais Obama amesema kuwa kifo cha Mandela kikumbukwe kwa kipindi cha maombolezo lakini pia kikumbukwe kwa kipindi cha kuhamasisha wakati watu wakitazama jinsi gani wanaweza kubadilisha maisha yao.
Rais Obama amefuatana na marais watatu wa zamani wa Marekani Jimmy Carter, George W. Bush na Bill Clinton,katika shughuli hiyo maalum.
Mandela anatarajia kuzikwa Jumapili Disemba 15 kijijini kwake Qunu. Via kiswahili.rfi.fr

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako