Amiri
Jeshi Mkuu ,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi Luteni usu
Evarist Mawalla wakati alipowatunuku Kamisheni maofisa wapya wa Jeshi la
Wananchi Tanzania baada ya kuhitimu mafunzo yao katika Chuo Cha Jeshi
Monduli Juu mjini Arusha jana.Luteni Usu Mawalla aliibuka mwanafunzi
bora katika mafunzo hayo yaliyochukua takribani mwaka mmoja ambapo
wanafunzi kutoka nchi za kigeni pia walishiriki.
Amiri
Jeshi Mkuu ,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi Luteni Usu
Immaculata Leodgar Mapunda baada ya kuibuka mwanafunzi bora wa kike
katika kozi ya maafiseshi la Wananchi wa Tanzania iliyofanyika Chuo Cha
Jeshi Monduli mjini Arusha jana.Katika mafunzo hayo yaliyochukua
takriban mwaka mmoja baadhi ya wanafunzi kutoka nchi za kigeni nao
walishiriki mafunzo hayo.
Amiri
Jeshi Mkuu ,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa hafla
ya kuwatunuku Kamisheni Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania
iliyofanyika Chuo Cha Jeshi Monduli mjini Arusha jana.Katika mafunzo
hayo yaliyochukua takriban mwaka mmoja baadhi ya wanafunzi kutoka nchi
za kigeni nao walishiriki mafunzo hayo.(picha na Freddy Maro)
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole na kumrekebisha tai mbunge wa
Monduli Mhe. Edward Lowassa ambaye juzi alinusurika katika ajali ya
ndege baada ya ndege aliyokuwa akisafiria inayomilikiwa na Shirika la
Ndege ya Precision kupasuka matairi yote ya nyuma wakati ikitua katika
uwanja wa ndege wa mjini Arusha. Rais Kikwete alikuwa Monduli Mkoani
Arusha kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi la Wananchi wa
Tanzania katika chuo cha jeshi Monduli.chanzo audiface jackson
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako