Katibu Mkuu
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa
----
Polisi mkoani Kigoma, imemshauri, Katibu Mkuu
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa
kusitisha ziara zake mkoani Kigoma kwa sababu za kiusalama.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Zedekia
Makunja alisema jana: “Ni ushauri tu tunatoa kwa Dk Slaa kwamba anaweza
kuahirisha kutokana na hali ilivyo hapa.” Hata hivyo, Kamanda Makunja
alisema pamoja na yote hayo bado Polisi mkoani, Kigoma imejipanga imara
kukabiliana na vurugu zozote zinazoweza kutokea katika ziara hiyo.
Lakini Dk Slaa alipoulizwa kuhusu ushauri huo
alisema hawezi kufuta ziara hiyo na kusema hahofii chochote. Alisema na
alishafahamu siku nyingi kuwa hayo yanayotokea. Juzi, vijana mbalimbali
waliandamana kwa pikipiki na wengine wakitembea kwa mguu huku wakiwa na
mabango kupinga ziara ya Dk Slaa Kigoma. Anatarajiwa kuwasili Kigoma
Kaskazini keshokutwa.
Sehemu ya Mabango yaliyobebwa a Vijana wapatao 10-15
Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa akihutubia katika Mkutano uliofanyika Kasulu, Kigoma
Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wlbrod Slaa akiwa na Wananchi wa Kijiji cha Kitanga, Kigoma.Picha na Chadema
----
Pamoja na Mbinu Chafu za Kutaka Kuvuruga Mkutano wa Chadema Kasulu Uliokuwa Unahutubiwa na Dr Slaa, lakini wananchi wengi wa Kasulu walijitokeza kumsikiliza Dr Slaa na kufurahishwa na hotuba yake iliyobeba maneno ya kuwapa Matumaini.
----
Pamoja na Mbinu Chafu za Kutaka Kuvuruga Mkutano wa Chadema Kasulu Uliokuwa Unahutubiwa na Dr Slaa, lakini wananchi wengi wa Kasulu walijitokeza kumsikiliza Dr Slaa na kufurahishwa na hotuba yake iliyobeba maneno ya kuwapa Matumaini.
Kulikuwa na kikundi cha Vijana wapatao kumi wenye mabango ambayo
yaliandaliwa mahsusi ili yatumike kuvuruga mkutano huo lakini mbinu zao
chafu zimeshindikana. Ili kuzima mipango yao michafu vijana hao walipewa
fursa ya kukaa mbele na mabango yao yenye ujumbe wa kuwaponda viongozi
wa Chadema.
Vijana hao walipewa fursa hiyo ili kuonyesha kwamba Chadema
kinaendeshwa kwa Demokrasia ya kumruhusu mwanachadema yeyote kutoa
mawazo yake anayopenda ili kudumisha Demokrasia ndani ya Chama.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako