Msanii wa hip hop nchini anaejulikana kwa
jina la WAKAZI leo asubuhi majira ya saa 12 wakati anarudi zake
nyumbani alinusurika kwa ajali mbaya ya gari kwa kugongwa na gari
nyingine maeneo ya Victoria. Wakati mimi na Pancho tunarudi nyumbani
tulikutana na ajali hiyo ikiwa ndio kama dakika 5 tu kutokea, dereva wa
gari aliyesababisha ajali hiyo alikuwa amelewa sana mpaka akawa
anashindwa kujielezea mwenyewe. Majira ya saa moja ndio waliweza kufika
mapolice na kupia ajali hiyo na hatimae magari hayo kubebwa na kupelekwa
Osterbay police. Kwenye ajali hiyo hakuna mtu yoyote aliyeumia.
Hii ndio gari ya Wakazi ikiwa imebebwa na
sehemu iliyoumia ni upande ule mwingine sehemu yote na milangoni na
tairi la nyuma lilipasuka.
Muda mfupi baada ya ajali hiyo Wakazi alipost hii status kwenye account yake ya Twitter. Pole sana ndugu yangu tuko pamoja.
Source: Dj Choka
Source: Dj Choka
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako