
Pichani ni ndege ambayo yaiendeshwi na binadamu maarufu kama Drones ( Unamanned aerial Vehicles) ambayo ni kati ya mbili zilizozinduliwa rasmi siku ya jumanne tayari kwa matumizi ya shughuli za ulinzi katika eneo la Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Anaonekena pia Mkuu wa Idara ya Operesheni ya Ulinzi wa Amani ya Umoja wa Mataifa ( DPKO) Bw. Herve Ladsous (katikati) akipewa maelezo kuhusiana na kifaa hicho. ( picha kwa hisani ya UN)
Na Mwandishi Maalum
Umoja wa Mataifa jana disemba tatu umetimiza azma yake ya kutumia teknolojia za kisasa katika operesheni zake za ulinzi wa amani baada ya kuzindua rasmi matumizi ya ndege maalumu ambao haziendeshwi na binadamu maarufu kama Drones au kwa jina la kitaalam ‘unamanned aeria vehichles ( UAVs).
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Umoja wa Mataifa, uzinduzi wa zana hizo umefanyika huko Goma ambako ni makao makuu ya Jimbo la Kivu ya Magharibi katika DRC na kushuhudiwa na watu wa kada mbalimbali wakiwamo baadhi ya viongozi wa juu wa Umoja wa Mataifa, serikali na waandishi wa habari.
Akinukuliwa wakati wa uzinduzi wa UAVs ambazo lengo lake ni kukusanya taarifa za kiitelejesia zitakazo saidia kutambua mapema hali ya hatari inayowakabili wananchi wa maeneo hayo na kutoa ulinzi na vile vile kubaini mienendo ya makundi ya wanagambo wenye silaha . Kiongozi mkuu wa Idara ya Operesheni za Kulinda amani za Umoja wa Mataifa ( DPKO) Bw. Herve Ladsous alikuwa na haya ya kusema
“ Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Umoja wa Mataifa ya matumizi ya teknolojia hizi za hali ya juu katika operesheni za ulinzi wa amani”. Na Kuongeza “Umoja wa Mataifa unahitaji kutumia aina ya zana hizi ili kutekeleza vema mamlaka zake”
Eneo la Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa muda mrefu limekuwa likikabiliwa na mapigano kati ya Mejeshi ya Serikali ya Kongo na makundi mbalimbali ya wanagambo wenye silaha likiwamo kundi maarufu la M23 linaloundwa na wanajeshi walioasi kutoka Jeshi la kitaita la DRC ( FARDC).
Kuzinduliwa kwa matumizi ya teknolojia hizo za kisasa, kunafuatia uamuzi wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa hasa kwa kuzingatia ugumu na ukubwa wa eneo ambalo liko chini ya mamlaka ya walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa kupitia MONUSCO
Mkuu wa DPKO Bw. Ladsous amefafanua zaidi kwa kusema kwa kuanzia ni drones mbili ambazo zitaanza kufanya kazi lengo likiwa ni kuwa na zana zaidi ya hizo kwa matumizi ya muda wote na kufanya kazi katika eneo kubwa.
Akifafanua zaidi Bw. Herve Ladsous amesema kwamba matumizi ya zana hizo umejidhirisha zaidi hususani katika siku za hizi karibuni ambao kundi la M23 limeanza kusambaratika kwa kile alichosema huenda kundi hilo limebaini kwamba kuna mabadiliko makubwa katika eneo hilo la Mashariki ya DRC hata kabla ya kuanza rasmi kwa matumizi ya zana hizo.
Naye Kamanda Mkuu wa MONUSCO Jenerali Santos Cruz yeyé amesema uwepo kwa aina hiyo ya teknolojia kutawawezesha kuchanganya taarifa zitakazokusanywa na zana hizo pamoja na zile zitakazo kusanywa na wataalamu walioko ardhini
Na kuongeza “ tutaweza kuchunguza mienendo ya makundi ya wanamgambo wenye silaha, na mienendo ya wananchi, tutaweza pia kuona silaha ambao zinabebwa na wananchi walioko ardhini, ni rahisi pia hata kuwaona watu walioko katikati ya misitu mikubwa, picha ambazo zinaweza kupatika hata katika umbali wa kilometa tatu”
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako