KULIA NI Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini , Suleiman Kumchaya....(picha aihusiani na taarifa hii bali ni kukupa taswira tu)
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini , Suleiman Kumchaya, ameingia kwenye kashifa nzito ya kumtapeli mama mmoja fedha taslimu kiasi cha Sh. milioni 50.
Kumchaya
ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke huyo
aliyejitambulisha kwa jina la Betty Matemba, anadaiwa kufanya utapeli
huo katika vipindi tofauti mara baada ya kushindwa ubunge 2010.
Akizungumza
na gazeti hili, Betty alisema Kumchaya wakati akiwa mbunge walikuwa na
uhusiano wa kimapenzi na walikuwa wakiishi kama mtu na mumewe.
“Unajua
huyu bwana alikuwa mshauri wa Rais Mkapa, baadaye aligombea ubunge
katika kipindi cha awamu ya kwanza ya serikali ya Rais Kikwete na
alishinda lakini awamu ya pili hakuweza kupata.
“Wakati
akiwa ni mbunge, bado alikuwa na uwezo mdogo sana kifedha,
alinishawishi kumkopea fedha benki lakini siku zinavyokwenda mwenzangu
hata halipi deni ndiyo nikachukua uamuzi wa kwenda bungeni ili akatwe
marupurupu yake ya ubunge lakini ikaonekana hakuwa na hata senti mmoja,”
alisema Betty.
Kwa
mujibu wa Betty, mkuu huyo wa wilaya alipomaliza kipindi chake cha
ubunge, maisha yake yakawa magumu kwani hakuwa na fedha wala mradi
ingawa alikuwa akimiliki mamia ya ekari.
“Anao
uwezo wa kunilipa, anazo ekari 60 za mikorosho Mtwara Vijijini, ekari
500 za ardhi huko Nachingwea akiziuza ni rahisi yeye kunilipa lakini
anachonifanyia ni uhuni.
Awali tulikubaliana anilipe fedha hizo ili nilipe madeni yote ninayodaiwa,” alisema.
Akiwa na makabrasha yanayoonyesha michanganuo ya fedha alizomtapeli, Betty anasema baada ya kupata ukuu wa wilaya alianza kumlipa kidogo kidogo ambapo Juni 28 mwaka jana alilipa Shilingi milioni moja na Julai 31 mwaka jana, alilipa Shilingi milioni moja na baada ya hapo hakuendelea tena.
Akiwa na makabrasha yanayoonyesha michanganuo ya fedha alizomtapeli, Betty anasema baada ya kupata ukuu wa wilaya alianza kumlipa kidogo kidogo ambapo Juni 28 mwaka jana alilipa Shilingi milioni moja na Julai 31 mwaka jana, alilipa Shilingi milioni moja na baada ya hapo hakuendelea tena.
Alisema
wakati fulani walishauriana yeye (Betty) na Kumchaya wanunue vigari
vidogo vya mizigo ili vimsaidie kusogeza maisha yake.
“Ilishindikana
kununua hiyo gari kwani fedha ninayoitegemea ndiyo hiyo… Jumamosi
(jana) kuna uwezekano wa kuondolewa kwenye nyumba niliyopanga Sinza
kwani nimepandishiwa kodi na sina uwezo,” alisema na kuongeza kuwa kodi
ya mwaka anatakiwa kulipia Sh. milioni 3.6 na kwamba mwenye nyumba
tayari ameshamkabidhi barua ya kuondoka.
Betty
alisema fedha hizo alitarajia kununua nyumba ambayo wakati huo ilikuwa
ikiuzwa Sh. milioni 70 lakini kutokana na ‘mheshimiwa’ huyo kumrubuni,
ilishindikana.
Alisema kutokana na jinsi alivyokuwa akimsumbua (Kumchaya) kulipa deni hilo, mkuu huyo wa wilaya alianza kutumia nguvu za giza.
“Kumchaya
akiwa na mkewe mwingine Mpemba na rafiki yangu mmoja na mumewe,
walikwenda Mbagala kwa mganga wa kienyeji wakitaka kuniua au kunifanya
kichaa.
“Huyu
mganga nilikuwa si mfahamu, lakini alipata namba yangu akanipigia
akitaka nimuone…nilikwenda na wifi yangu (dada yake Kumchaya),
tulipofika alinieleza yote pamoja na fedha aliyolipwa...," alisema.
Dada yake Kumchaya , alilipopigiwa simu kutoka Masasi, alikiri kutambua uhusiano uliopo wa Betty na Kumchaya.
“…huyu Betty ni wifi yangu kabisa, mkewe Selemani, ni wifi yangu ninayempenda sana.
Ni kweli Kumchaya na mkewe Fatma walikwenda kwa huyo mganga huko Dar es Salaam wakitaka kumroga Betty.
Huyu mganga alimvuta Betty kimadawa hadi alipompata na siku hiyo tulikwenda wote kwa huyo mganga. Betty Mungu anampenda sana...," alisema Mwajuma kwa lafudhi ya Kimakonde.
Huyu mganga alimvuta Betty kimadawa hadi alipompata na siku hiyo tulikwenda wote kwa huyo mganga. Betty Mungu anampenda sana...," alisema Mwajuma kwa lafudhi ya Kimakonde.
Miongoni
mwa fedha ambazo Betty anadai kuzikopa kwenye taasisi za fedha kwa
ajili ya kumridhisha Kumchaya ni pamoja na Shilingi milioni saba (NMB),
Shilingi milioni tisa (International Bank), Shilingi milioni 10 (Akiba
Commercial) na Shilingi milioni 4.2 (Vission Saccos), hizo ni mbali na
zile alizokopa kutoka kwa watu binafsi.
“Ilifikia
kipindi aliniomba nikope Sh. milioni tisa kwa ajili ya kufanyia harusi
ya mtoto wake, nilifanya hivyo na harusi ilikuwa nzuri sana.
Nilipoona hana muelekeo wa kulipa madeni hayo ilibidi tuandikishiane,” alisema huku akionyesha nyaraka hizo.
Betty
anasema pamoja na kumuitia wazee wa heshima na viongozi wa dini ya
Kiislamu ili wazungumze na Kumchaya alipwe deni lake, ilishindikana
kabisa.
“Mimi sina ugomvi na huyu bwana, ninachotaka anilipe deni langu tu ili tuishi kwa amani,” alisema.
Mkuu
wa Wilaya, Kumchaya alipotafutwa kwa siku tatu mfululizo kwa simu akiwa
Tabora, alisema yuko kwenye kikao apigiwe baadaye lakini alipopigiwa
simu yake ilikuwa ikiita bila majibu.
“Unajua huyu mwanamke anakichaa…subiri niwasiliane na mwanasheria wangu nipigie baadaye,” alisema.
Hata hivyo, mwandishi wa habari hizi alipoendelea kumpigia simu yake ya mkononi, iliita bila majibu.
CHANZO: NIPASHE Sunday Dec 15, 2013
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako