Naibu Waziri wa mawasiliano, Sayansi na Teknologia, Mhe. January
Makamba akiwa na mkewe Ramona Makamba wakipokewa na Afisa Ubalozi Mindi
Kasiga(wapili toka kushoka) na mwenyekiti wa Vijimambo Baraka Daudi mara
tu walipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling,
Virginia. Mhe. Makamba amekuja maalum kama mgeni rasmi kwenye sherehe
ya Uhuru wa Tanzania itakayofanyika Jumamosi Desemba 7, 2013 Laurel,
Maryland nchini Marekani.
Afisa Ubalozi Mindi Kasiga akimweleza jambo Mhe. January Makamba
wakati alipokwenda kumpokea uwanja wa kimataifa wa Dulles uliopo
Sterling, Virginia.
Mheshimiwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwenye
picha ya pamoja na Makatibu Wakuu na Maafisa wa Ubalozi. Kutoka kushoto
ni Bw. Paul Mwafongo (Kaimu Balozi), Bw. George Yambesi (Katibu Mkuu
Utumishi), Mhe. January Makamba, Bw. Peter Ilomo (Katibu Mkuu Ikulu),
Bw. Suleiman Saleh (Kaimu Mkuu wa Utawala).
Mhe. January Makamba Picha ya pamoja na Ujumbe wa PSPF wakiwemo maafisa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Mhe. January Makamba na mkewe Ramona wakibadilishana mawili matatu na
Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mindi Kasiga.
Kutoka kushoto ni Afisa Ubalozi Abbas Missana, Afisa Ubalozi Mindi
Kasiga, Ramona Makamba na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknologia, Mhe. January Makamba wakiwa kwenye maongezi.




No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako