Akimnyooshea
kidole, acha mambo yako mwana!: Per Mertesacker (kulia) akimuwakia
Mesut Ozil baada ya kula kipigo cha mabao 6-3 kutoka kwa Manchester
City
KIPIGO siku zote kinavuruga!!. Baada ya Arsenal kuburuzwa kwa kipigo cha mabao 6-3 kutoka kwa Manchester City, Wachezaji wawili wa klabu hiyo raia wa Ujerumani, Per Mertesacker na Mesut Ozil wamepigana mkwara mzito wakati wakitoka nje ya uwanja wa Etihad.
Mertesacker
alimuwakia vikali Ozil ambaye ni rafiki mkubwa katika soka na
kumnyooshea kidole kiungo huyo baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa.
Hali hiyo imetokea baada ta Ozil kushindwa kuwapungia mkono wa heshima mashabiki wa Gunners waliosafiri ugenini.
Wakati
wawili hao wakizozana, kocha mkuu wa klabu hiyo, Arsene Wenger alicheka
tu na kusema: “Waache Wajurumani, watamalizana wenyewe, msijali”.
Mabao
ya City yamefungwa na Sergio Aguero dakika ya 14, Alvaro Negredo dakika
ya 39 Fernandinho mawili dakika za 50 na 88 David Silva dakika ya 66 na
Yaya Toure dakika ya 90.
Theo
Walcott alirejea uwanjani kwa mara ya kwanza leo tangu Septemba na
kufanikiwa kutundika nyavuni mabao mawili ya Arsenal dakika za 31 na
63, wakati lingine lilifungwa na beki Per Mertesacker dakika ya 90.
Acha hizo!: Mertesacker akiendelea kumuwakia rafiki yake mkubwa katika soka
Wakionesha mfano: Jack Wilshere (kushoto) na Mertesacker wakionesha heshima kwa mashabiki waliosafiri leo
Katika
mechi nyingine leo, Fernando Torres alifunga bao mojawapo katika
ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace na kuifanya Chelsea iwe
nyuma kwa pointi mbili na vinara Asernal ambao leo wamekula kisago
kikubwa kutoka kwa Man City.
Bao
lingine la Chelsea limefungwa na Mbrazil, Ramirez katika dakika ya 35
akipokea pasi kutoka kwa Eden Hazard. Bao la kufutia machozi kwa Crystal
Palace limefungwa na mashambuliaji wake raia wa Morocco, Marouane
Chamakh.
Kocha
Jose Mourinho anaamini kuwa haiwezekani hata kidogo kuwafananisha
washambuliaji wake na vijana wenye kipaji kikubwa na maarifa ya soka wa
klabu ya Man City, Sergio Kun Aguero au Luis Suarez wa Liverpool.
Kupingana
na mtazamo wa kocha wake, Torres alifunga bao la kwanza ambalo
linamaanisha Chelsea watakwea kileleni kabla ya krimasi endapo
wataifunga Arsenal katika dimba la Emirates desemba 23 mwaka huu.
Ramires aliifungia Chelsea bao la pili
Kikosi
cha Chelsea: Cech 5; Ivanovic 6, Luiz 6, Terry 6, Azpilicuta 7; Essien
6, Ramires 7; Willian 7 (Schurrle 82), Mata 5 (Oscar 62, 5), Hazard 6;
Torres 5 (Ba 84).
Crystal
Palace: Speroni 8; Mariappa 6, Gabbidon 7, Delaney 6, Ward 7; Bannan 5
(Bolasie 51, 5), Jedinak 7, Dikgacoi 5 (O’Keefe 26, 7), Puncheon 6;
Chamakh 7 (Gayle 88), Jerome 7.
Shock on the cards: Marouane Chamakh continues his good form infront of goal by making it 1-1
Amerudi mchezoni: Chamakh akirudisha matumaini kwa Palace baada ya kusawazisha na kufanya ubao usomeke 1-1
Mourinho naweza baba!: Fernando Torres akishangilia bao la kwanza dhidi ya Palace
Mechi zilizomalizika matokeo yako ifuatavyo;
England: Premier League
Finished
|
Manchester City
| 6-3 |
Arsenal
| (2-1) | ||||||
Finished
|
West Ham
| 0-0 |
Sunderland
| (0-0) | ||||||
Finished
|
Newcastle United
| 1-1 |
Southampton
| (1-0) | ||||||
Finished
|
Everton
| 4-1 |
Fulham
| (1-0) | ||||||
Finished
|
Chelsea
| 2-1 |
Crystal Palace
| (2-1) | ||||||
Finished
|
Cardiff
| 1-0 |
West Bromwich Albion
|
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako