A

A

Mechi ya Stars na Kenya yaahirishwa, uwanja wa machakos haufai, ni majaruba ya mpungA

Hii ndiyo hali halisi ya Uwan
Katibu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye amesema kwamba sababu ya kufikia hatua hiyo ni hali mbaya ya Uwanja wa Kenyatta kufuatia mvua kubwa iliyonyesha leo. Makocha wa timu zote, Kim Poulsen wa Tanzania Bara na Adel Amrouche wa Kenya wamekagua Uwanja na kujiridhisha haufai kuchezewa, ingawa Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Kenya (FKF) alikuwa anashinikiza mechi hiyo ichezwe hapo hapo. Lakini pamoja na Musonye kutoa uamuzi huo,  Nyamweya amewaamuru wafanyakazi wa Uwanja wachote maji uwanjani aking’ang’aniza mechi ichezwe hapo.
Amrouche kushoto akimbishia Nyamweya mbele ya Musonye

Kim Poulsen ameweka msimamo hachezi Kenyatta



Musonye akiwapa taarifa rasmi kocha Kim na Mkuu wa Msafara wa Stars, Msafiri Mgoyi kwamba mechi ni Nairobi



Hatuingizi timu mtaalamu mwenzangu hapa; Amrouche kushoto akizungumza na Kim

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako