A

A

Mbakaij sugu akamatwa kwa kumbaka na kumlawiti mwanafunzi hadi akazimia


Habari na Joseph Ngilisho, Arusha — Kinara sugu wa ubakaji ,Selemeni Said(30) mkazi wa Mbauda jijini hapa,amenusulika kufa kwa kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali baada ya kufumwa, akiwa na wenzake wakimbaka mwanafunzi wa kidato cha pili na kumsababishia kupoteza fahamu.

Saidi anayetajwa kuwa mwenyekiti wa kundi la wabakaji, alishambuliwa na wananchi hao baada ya kukutwa kwenye nyumba inayodaiwa kuwa danguro la uhalifu eneo la Muriet, Bon city jijini hapa, wakimwingilia kinyume na maumbile mwanafunzi mwenye umri wa miaka14, hata hivyo polisi walimwokoa na kipigo hicho na kumfikisha kituoni.

Mashuhuda wa tukio hilo, akiwemo mwenyekiti wa mtaa huu, Francis Mbise walielezwa kuwa mtuhumiwa huyo akiwa na 
wenzake watano, walimbaka  usiku kucha msichana aliyetajwa kwa jina moja la Jacqueline mkazi wa kwa Morombo baada ya kufanikiwa kumrubuni na kumwingiza kwenye nyumba hiyo na kumfanyia kitendo hicho.

Hata hivyo mnamo majira ya alfajiri  mtuhumiwa alionekana akitoka kwenye nyumba hiyo akiwa kifua wazi akikimbia, ndipo wananchi walipomtilia shaka na kumkimbiza ambapo walipomkamata na kumhoji, alisema yeye sio mwizi ila alikuwa akifanya mapenzi na msichana.

Mbise alisema kuwa baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa, wananchi waliongozana haye hadi kwenye nyumba hiyo na kukuta msichana huyo akiwa amelala hajitambui huku sehemu zake zake mbili zikitoka damu, ndipo wananchi hao walipoamua kumshushia kipigo cha nguvu kabla ya polisi kufika na kuokolewa.

Mwenyekiti alisema baada ya kumhoji mtuhumiwa huyo sababu ya kutimua mbio alisema kuwa yeye na wenzake walihofu kuwa msichana waliyembaka amepoteza maisha, baada ya kushtuka usingizini na kukuta msichana huyo akiwa hajitambui huku wenzake wakiwa hawapo, ambapo alipoamua kuondoka kwa hofu ya kukutwa na kukamatwa.

Alisema mtuhumiwa huyo alikiri kuunda kundi la ubakaji lenye watu watano likiongozwa na yeye huku wakigeuza makazi ya mmoja wa wahalifu hao kuwa danguro la ubakaji. Hata hivyo watuhumiwa wengine walifanikiwa kukimbia na kutotambulika na wananchi wanaendelea kuwasaka: ‘Vvitendo vya ubakaji vineshamiri sana eneo hilo na tulikuwa hatufahamu hawawabakaji wako wapi maana kila siku taarifa za kubakwa ninasikika huku taarifa vza wabakaji zikibaki siri ila leo tumemnasa kinara wao na wengine tunawasaka ili tukomeshe kabisa matukio hayo.

Mtuhumiwa huyo alichukuliwa na polisi wenye silaha na kupakiwa kwenye gari aina ya Landrover lenye namba PT 1177 huku akiwa ametapakaa damu nyungi usoni zilizotokana na kipigo kutoka kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako