Hawa ni wazee wa zamani ambao sasa ni walimu wa mchezo wa Ngumi, Wakati wao ndio walikuwa Mabondia Wakubwa
Wapigangoma wa Kikundi cha Ngoma ya Mchiriku cha Jagwa wakitumbuiza katika Bonanza la Masumbwi
Mwimbaji wa Kundi la Jagwa akitumbuiza vilivyo katika Bonanza hilo la Masumbwi.
Afisa habari wa Shirikisho la Ngumi Tanzania Salim Mwiduka akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa Bonanza la wazi la ngumi.
Mwenyeji wa Maandalizi ya Bonanza la Ngumi Kessy Juma akiwa anafungua Bonanza hilo.
Mwenyekiti wa kamati ya Tuzo za ngumi Said Masanga akielezea juu ya Tuzo hizo za ngumi.
Mjumbe wa Shirikisho la Ngumi wanawake Bi. Aisha George Vaniatis akiwa anafuatilia mpambano
Kulia ni Mwalimu mkongwe wa Mchezo wa ngumi bwana Rashid au anafahamika kwa jina la
Super D
Mpambano
wa kwanza kati ya Gervas Rogiansion aliyevaa gloves nyekundu akipambana
vikali na mpinzani wake John Christian aliyevaa Gloves za rangi ya bluu
, ambapo John Christian aliibuka mshindi kwa Makonde mawili kwa moja.
Umati wa watu waliojitokeza kutazama Bonanza la wazi la Ngumi katika kituo cha mabasi cha Mwenge
Mashabiki wa Ndondi wakishangilia
Mpambano
wa pili kati ya Haruna Swanga aliyevaa gloves nyekundu aliyepambana
vikali na na mpinzani wake Kulwa Makenzi aliyevaa Gloves za
rangi ya bluu , ambapo Haruna Swanga aliibuka mshindi kwa kumtandika
mpinzani wake makonde matatu kwa sifuli.
Mpambano wa tatu kati ya George Costantino aliyevaa gloves nyekundu
aliyepambana vikali na na mpinzani wake Hamadi Furahisha aliyevaa Gloves
za
rangi ya bluu , ambapo Hamadi Furahisha aliibuka mshindi kwa kumtandika mpinzani wake makonde mawili kwa moja.
Leonard
Machichi aliyevaa gloves nyekundu akiwa anajikimu kukwepa ngumi kutoka
kwa mpinzani wake Abuu Bakari wakati wa mpambano huo
Abuu Bakari akipokea kipigo cha nguvu kutoka kwa mpinzani wake Leonard .. ambapo hali ilikuwa mbaya sana kwa Abuu
Mwamuzi
wa Mpambano huo Michael Mwamkenja akisimamisha mpambano huo katika
Mzunguko wa pili baada ya Bondia Abuu kunyosha mikono juu ishara ya
kushindwa .
Leonard Machichi akitangazwa mshindi wa pambano hilo kali ambalo wanaliita RDT
Makamu
wa Raisi mpya wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania Lukelo Anderson
au Man Power akiwa anatoa Neno la Shukurani Mara baada ya mpambano huo
kuisha.
Kutoka
Kushoto ni Bi. Zuena Kipingu ambaye ni Mjumbe wa Maendeleo ya Vijana na
wachezaji katika Shirikisho la ngumi za Ridhaa Tanzania,Mutayoba
Rwakatale Katibu wa maandalizi hayo, na Bondia Haruna Swanga.
Picha zote na Dar es salaam yetu.
Shirikisho la ngumi
(BFT) lazindua rasmi mashindano ya ngumi jijini da es salaam ni baada ya
siku ya jana kufanya uchaguzi wa makamu mwenyekiti ambaye aliweza kuchaguliwa na kupita kwa
kishindo Bw.Lukelo andasoni aanza
kuonyesha umahiri wake katika kazi
Akifungua mashindano hayo Bw.Kesi juma ambaye ni muandaaji
wa mashindano hayo akishirikiana na wanakamati ya maandalizi akiwemo mwenyekiti
wa kamati hiyo Bw.Saidi Masanga paoja na makamomwenyekiti Bw.Muta YobaLwakatale
amesema wameweza kuweka hadharani ili kuwahamasisha watu waweze kuwa na imani
na mchezo huo wa ngumi pamoja na kuwapa burudani
Aidha Bw.Kesi Juma amesema kuwa vijana wengi wanauwezo
wakukabiliana na tatizo la ajira kwa kujiingiza katika mchezo huu ameweza ku
taja baadhi ya faida zinazo patikana katika mchezo wa ngumi ni pamoja na
kuimarisha afya,ajira ya kudumu na
kuweka akili katika wakati wa kufikiria
,baada ya hapo ndipo alipo karibisha rasmi mapambano kuweza
kuendelea .Ambapo waliweza kuandaa mapambano manne(4) yenye uzito tofauti makundi mawili yenye uzito wa kilo (91) na
LIngine likiwa na uzito wa kilo ((52) pamoja na lenye uzito wa kilo (49) kila
kundi likipewa mizunguko mitatu yenye dakika (5)
Makundi na matokeo
Kundi la kwanza likiwa linaanza walipambana Gervas
Rogiansino akirushiana makonde na John
Christian wote wakiwa na uzito sawa wa kilo (49) ambapo john katika mizunguko yote alimshambulia gervasi
na kuweza kuibuka kinala wa mchezo kwa kumchapa makonde (2) kwa (1)
Kundi la pili liliingiauwanjani kwa mbwembwe wakiwa wote ni
wenye uzito wa kilo (91) ambapo walikuwa wakipambana vinara wawili wa masumbwi
ambao ni Haruna Swanga baina ya Kulwa makenzi,Kwa mizunguko yote walionekana
wakishambuliana kwa kasi huku Haruna
akionekana kumtupia makonde zaidi adui yake nahivyo kumfavya akose uwiano na
kumzidi kete hatimaye Haruna Kuondoka na
ushindi Wa Kumtandika makonde(3) kwa (0)
Awamu ya tatu ilianza wakiwa wanapambana George Costantino
na Hamadi Furahisha ambapo wakiwa na uzito wa kilo (52) waliweza kuumudumchezo
kwa mizunguko miwili ndipo Hamadi alipo bahatika katika mzunguko wa tatu kwa
kuzidiwa konde mojalililo mpelekea kushindwa kwa makonde (2) kwa (1)
Mzunguko wa misho uliwadia baada ya muda huku umati wa watu
uliofika hapo ukiwa unashauku kubwa ya
kuweza kutambua ninani atakaye mtanga mwenzake kati ya Reonard Machichi na Abu
au Bakari Mpambano wa wanamasumbwi hao ulianza huku (Refa) akiwa ni Maiko
mwankenja akiwajibika kuwaongoza mabondia hao mzunguko wa kwanza ulimalizika
vizuri kasheshe ilianza katika mzunguko wa pili wakati Reonard alionekana
kumshambulia kwa kasi Abu na kuishiwa pumzi hari hiyo ilipeleka Mwanamasumbwi
Abu kushindwa kuendelea na mpambano kwa kunyosha mikono yake juu ishara ya
kuomba msaada harihiyo kwa wana masumbwi inaitwa (RDT)ambapo refa alichukua
uamuzi wa busara na kumtangaza Reonard Machichi kuibuka na ushindi.
Baada ya kumalizika kwa michzo hiyo Tone
multimediaikiwakilisha da es salaam yetu ilifanikisha kuzungu mza na baadhi ya
washiriki na watazamaji walio fika kuhudhuria mchezo huo mshiriki mmoja alisema “hii ni moja ya burudani na ni ajira hususani kwa sisi vijana tunao
lia na ajira kila si natoa wito kwa vijana wezangu waweze kuthubutu
wataweza”huyo ni George costantino ,na watazanaji walikuwa na haya ya kusema
juma isa “nimeweza kushawishika kuja kuangalia live ngumi zinavyo tupwa na
kujifunza wameniburudisha nah ii ni fursa lazima niitumie “, Rashid amadi
“ninashukuru kwa kutuhamasisha kwakuwa hatukujua kuwa hata ngumi ni ajira yenye
manufaa hapa duniani kwa leo nimejifunza mengi ukizingatia ni siku ya ukimwi
duniani watu wamefika kwa wingi ili waone maonesho haya”
Wakati wa kufunga maonesho hayo Mwenyekiti wa kamati ya
maandalizi aliweza kutambulisha baadhi ya viongozi walio weza kufika
katika uzinduzi huo wakiwa ni wapya kwa
upande wa wana wake alikuwepo mjumbe wa maendeleo na vijana na wachezaji wa
ngumi za ridhaa Bi.zuena Kipingu ambaye alikuwa na haya ya kuzungumza kwa
wazazi na vijana waweze kuwaachia watoto na wasifikirikuwa ngumi ni uhuni bali
ni mchezo wa kawaida wenye kipato kikubwa alitoa wito na kumkaribisha
mwanamasumbwi bingwa wa Champion Ambaye ni mwanake ABDU ZUGO ambaye alisema
amepata mafanikio makubwa kupitia
ndondi.Njumbe mwingine aliye chaguliwa Bi.Aisha George Vaniatis ambaye
ni mjumbe wa shirikisho la ngumi wanawake.
Pambno
la kwanza
|
Gervas
Rogianso
Vs
John
Christian
|
Mizunguko
(3)
|
-Gervas
Rogianso(1)
John
Christian(2)
|
Mshindi
John
Christian(2)
|
Pambano
la pili
|
Huruma
Swanga
Vs
Kulwa
Makenzi
|
Mizunguko
(3)
|
Huruma
Swanga
(3)
Kulwa
Makenzi(0)
|
Mshindi
Huruma
Swanga
|
Pambano
la tatu
|
George
costantino
Vs
Hamad
Furahisha
|
Mizunguko
(3)
|
George
costantino(2)
Hamad
Furahisha(1)
|
Mshindi
George
costantino
(2)
|
Pambano
la nne
|
Reonard
Machichi
Vs
Abu
au Bakari
|
Mizunguko
(3)
Mmoja
hakumaliza
|
RDT
|
Mshindi
Reonard
Machichi
(RDT)
|
MICHUANO ILIVYO KUWA
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako