Hafla ikiendelea katika ukumbi wa Victoria Palace Hotel jijini Mwanza. |
Meneja wa The Great Zone Entertainment Albert G. Sengo (kushoto) akitoa matarajio ya Kampuni. |
Baadhi ya Maaskofu. |
Bahati Bukuku naye alikuwa sehemu ya waalikwa kwenye hafla hiyo. |
Sala ya kuhitimisha hafla. |
Naibu Waziri wa wizara ya Sayansi na Teknolojia Januari Makamba akizungumza na wanahabari mara baada ya kumalizika hafla hiyo. |
MWANZA:Naibu
Waziri wa wizara ya Sayansi na Teknolojia Januari Makamba amesema taifa
lipo katika kipindi Kigumu hivyo kuwataka maaskofu na wachungaji wa
makanisa mbalimbali nchini kuiombea nchi yetu ili ipate kiongozi mwenye
sifa zinazotajwa katika Biblia.
Akizungumza kwenye Hotel ya Victoria Palace katika Hafla ya chakula cha
usiku kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa mbalimbali ya iliyoandaliwa
na Kampuni ya The Great Zone Entertainment, inayoshughulika na
matamasha ya muziki wa Injili na sanaa, alisema ameamua kusema hayo
mbele ya Maaskofu na Wachungaji ambao aliwaita watu wazito wenye
kuaminiwa na kuheshimiwa katika jamii.
Hafla hiyo iliudhuriwa na Askofu Zenobius Isaya ambaye ni makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa ya Kikristo mkoa wa Mwanza, Askofu
Alex Mwakisumbwa mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentokosti (P.C.T) pamoja
na Askofu Charles Sekelwa ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa makanisa ya
Kikristu mkoani Mwanza.
“Taifa linapita katika kipindi kigumu, linajaribiwa linapita kwenye
wakati mgumu, ….Ndugu zangu yakusema yapo mengi, lakini nadhani
tuzungumze machache yanayohusu nchi yetu na Taifa letu, kwa sababu wote
ni watanzania hapa na wote tuna hamu ya kujua na kutafakari mustakabali
wa nchi yetu, umoja wetu, amani yetu na utulivu wetu,” alieeleza.
Alisema nchi yetu inahitaji kuponywa, ili ianze upya (Reset) na
kubainisha kuwa katika kuanza upya kama Taifa linahitaji aina ya
viongozi wenye sifa za kama za viongozi wa dini ambazo zimebainishwa
ndani ya Biblia na jukumu hilo kuhakikisha akiongozi wa sifa hizi
anapatikana wqanalo wachugaji.
“Taifa lipo katika changamito kama rushwa, wizi, ubakaji, kumomonyoka kwa maadili na ninyi viongozi wa dini mnaziona na kukabiliana nazo kila
siku, jamii yetu hii kwa sasa uongo umzidi, ubakaji umezidi, wizi
umezidi mauaji yamezidi sasa nini kinaendelea na kutokea na kwa nini
maovu yanaongezeka juu yetu?” alihoji Makamba.
Alisema katika hali kama hii kuna kipindi Mungu hukasirika na kutoa
adhabu, hivyo kutaka Gharika pamoja na Sodoma na Gomola zilikuwa ni
adhabu za Mungu kutokana na watu kupitiliza katika maovu hivyo adhabu ya
kwanza ilikuwa ya Maji na ya pili ilikuwa Moto, hatujui inayofuata kwa
nchi yetu itakuwa ya nini, japo kama Taifa hatutegemei kufuka huko.
Alieleza kwamba moja kati ya ujumbe wake kwa viongozi hao ni kama kizazi
cha sasa ama taifa tunahitaji uponyaji wa hali ya juu na kwamba katika
uponyaji huo viongozi wa dini wanayo nafasi kubwa sana ya kuiponya nchi
hii ili iepuke adhabu kama za nyakati hizo zilizotolewa na Mungu.
“Shughuli za siasa zimeingiliwa na Matapeli, lakini hata shughuli yenu
pia imeingilia na matapeli vilevile sasa tunapotafuta uponywaji wan chi
yetu ninyi mnanafasi kubwa sana kwani uponyaji tunaoongea ni wa maovu ya
kiroho, uongo ubakaji na vitu kama hivyo, ninyi mnanafasi kubwa sana.
Viongozi wa siasa pia tunayo nafasi wote tunanafasi lakini ili
tufanikiwe na nchi ipone lazima viongozi wa siasa wawe wasafi,”
alieleza.
Alisema Askofu ama mchungaji akihubiri anapaswa kuwa msafi, na hata
katika uongozi wa siasa anaposimama mtu na kusema yeye ni jawabu la
matatizo ya wananchi ama yeye ni nyezo ya matatizo ni vizuri kumtazama
sura yake kama ameacha (maovu).
Tunapoomba uongozi wa kisiasa zipo sifa kwani tunaomba kuongoza watu wa
mungu ambao ni wale wale wanaokuja Makanisani ndiyo wanaokuja katika
siasa, kuongoza watu wa mungu siyo kitu kidogo maana hata mamlaka ya
serikali yametambuliwa hivyo lazima vigezo vya kuongoza watu hawa view
vikubwa sana.
“Katika Biblia zinataja sifa za mtu atendae kazi ya Askofu ngoja nizisome (1 Timotheo 3.1) zinasema
… mtu akitamani kazi ya Askofu, atamani kazi nzuri. Basi, imempasa
askofu awe mtu asiye na lawama, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi,
anayejitawala, anayeheshimika, mkarimu, ajuaye kufundisha. Asiwe mlevi,
wala mkali bali awe mpole, asiwe mgomvi wala mpenda fedha,” alisema na
kuongeza katika siasa hatutafuti askofu lakini ni lazima sifa zifanane
na hizi za askofu na kuwataka viongozi hao wa makanisa kuzisoma sifa
hizo kila watu wanapopita kwao kutafuta uongozi wa nchi na kila mtu
anayetafuta uongozi lazima ajipime kwa sifa hizi.
Alisema hata hivyo kumekuwa na mjadala mkubwa wa sifa za uongozi kuhusu
kijana, uzoefu na kubainisha kwamba amekuwa akitoa mwito kwa vijana
ambao hawana makandokando washiriki na kujitokeza katika kusaidia nchi
ipone.
Makamba aleleza vijana wengi wamekuwa waoga waoga, wengi wamekuwa
wakidai kutokuwa na fedha, uzoefu lakini maaskofu na wachungaji
wanapaswa kuwa mashahidi kupitia vitabu kwani katika Yeremia imeelezwa
jinsi Mungu alivyompatia unabii Yeremia ambaye alidai yeye bado mdogo na
siwezi.
“Yeremia alipopewa unabii alilalamika mimimi mdogo mimi siwezi, lakini
mungu alimwambiaje, ngoja nisome, (Yeremia 1: 4-10) ….Kabla sijakuumba
ndani ya tumbo la mama yako nilikujua, kabla hujazaliwa nilikutenga kwa
kazi maalumu, nilikuweka uwe nabii kwa mataifa,” alifafanua na kuongeza
kuwa bwana alimwambia “Usiseme, ‘mimi ni mtoto mdogo. Utakwenda popote
nitakapokutuma na kunena lo lote nitakalokuagiza, usiwaogope, kwa maana
niko pamoja nawe nikuokoe.”
Kutokana na kauli hiyo ya Januari Makamba Askofu Jacoub Lutabija alisema
amepokea ujumbe mzito ambao atakwenda kuutangaza kwa waumini wake
Musima na kubainisha kwamba kwa ujumbe huo watu wenye hekina zao
wametambua nini wanapaswa kufanya.
“Haya ni maneno mazito, mimi nimefurahi sana na nimueleze mgeni wetu
nitakwenda Musoma kuwaeleza watu wangu juu ya ujumbe huu wenye maana
sana kwa mustakabali wan chi yetu,” alisema.
Kwa upande wake Bahati Bukuku msanii wa Nyimbo za Injili, yeye aliwaasa
wachungaji kuacha kuomba na kufunga mambo yanapokuwa mabaya kwani tatizo
linaanzia pale maono yanapopuuzwa hivyo kuwataka kuangalia namna ya
kuunga mkono kauli zenye maono kama hayo ambayo yanasaidia kuokoa nchi.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako