Mwenyekiti
wa Asasi ya vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA), Dr. Lwidiko
Edward, akizungumza na vijana kutoka Asasi mbalimbali hapa nchini juu ya
ushiriki wa vijana katika mkutano uliopita wa COP 19 katika ukumbi wa
mikutano wa Ofisi UNESCO jijini Dar es Salaam.
.Mvua na mafuriko ni mifano hai katika baadhi ya nchi duniani
.Mapigano ya wakulima na wafugaji ni madhara ya mabadiliko ya tabianchi
Na Damas Makangale, MOblog
CHAMA
CHA UMOJA WA MATAIFA CHA VIJANA (YUNA) kimesema kwamba mvua, mafuriko
na mapigano ya wakulima na wafugaji yanasababishwa na mabadiliko ya
tabianchi na kuomba nchi wanachama kuja na mpango mkakati wa muda mrefu
kukabiliana na majanga hayo.
Akizungumza
na vijana kutoka Asasi mbalimbali za vijana nchini kwenye mkutano wa
kujadiliana yaliyojiri katika mkutano wa 19 wa mabadiliko ya tabianchi
(COP 19) uliofanyika Warsaw, Poland Afisa Mradi wa Jukwaa la Mabadiliko
ya tabianchi, Fazal Issa, amesema kwamba mabadiliko ya tabianchi
yamesababisha hasara na vifo kutokana na mvua kubwa zinazosababishwa
mabadiliko hayo ya tabianchi.
“kwa
mantiki hiyo wanachama kutoka nchi 194 kwenye mkutano wa COP 19 nchini
Warsaw, Poland walikubaliana kuja na mkakati wa muda mrefu kushughulikia
mabadiliko ya tabianchi yanayosababisha mvua na mafuriko sehemu nyingi
duniani,” amesema.
Afisa
Mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi, Fazal Issa, akiwasilisha ripoti yao
ya ushiriki wa vijana na mambo waliokubaliana na wanachama na Asasi za
kiraia katika kupambana na mabadiliko ya Tabianchi na umuhimu wa
kupunguza hewa ukaa duniani.
Issa
amesema kwamba moja ya makubaliano ya mabadiliko ya tabianchi ni kuja
na mkakati wa teknolojia na habari ili kuweza kupiga hatua katika
kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia teknolojia zaidi
kupunguza hewa ukaa kwenye anga ya duniani.
Amesema
pia kwamba katika mkutano huo wajumbe walikubaliana katika kutengeneza
mfumo wa kifedha wenye kuwezesha kamati na tume mbalimbali za kupambana
na mabadiliko ya tabianchi kwa kuchangisha fedha kutoka kwa wanachama
mbalimbali duniani.
“mpaka
sasa kamati ya utendaji wa mabadiliko ya tabianchi imeshakusanya karibu
Tsh 33 billioni katika kushughulikia matatizo ya mabadiliko ya
tabianchi duniani,” alilisitiza
Mkuu
wa kitengo cha Model UN-YUNA , Adam Anthony, akizugumzia ushiriki wa
vijana na Asasi za kiraia katika mkutano wa COP 19 uliofanyika nchini
Poland na umuhimu wa wanachama kukubaliana kupunguza hewa ukaa wa
maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Asasi ya vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA), Dkt. Lwidiko Edward ,
amesema wamekuja na mkakati wa kutoa taarifa kwa vijana wenzao ya juu
ya yaliojiri katika mkutano wa tabianchi na nafasi ya vijana katika
kupambana na matatizo ya tabianchi duniani.
Dkt.
Edward, aliongeza kuwa katika mkutano wa COP 19 vijana waliweza
kushiriki kikamilifu katika kupeleka agenda zenye maslahi mapana kwa
vijana na vizazi vijavyo na madhara ya mabadiliko ya tabianchi kwa
vijana duniani.
“wanachama
wa mabadiliko ya tabianchi duniani wamekubaliana kupunguza hewa ukaa
ili kupunguza joto duniani kwa kuanzia ni kwenye nchi zenye viwanda
vingi,” amesema.
Amesema
pia mabadiliko ya tabianchi katika nchi zinazoendelea inaonekana
dhahiri kwenye sehemu zenye ukame kwa sasa na mapigano ya wafugaji na
wakulima ni mifano hai ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi katika nchi
zinazoendelea.
Dkt.
Edward, amesema kwamba kupunguza hewa ukaa duniani ni muhimu hata kama
baadhi ya nchi tajiri zinategemea viwanda katika kukuza chumi zao na
kuleta maendeleo kwa watu wao.
Vijana wakiuliza maswali mbalimbali juu ya ukweli kwamba Je sauti ya vijana inasikika katika mikutano ya COP duniani.
Allyah
Mohammed kutoka YUNA, akizungumza kuhusu swala la jinsia na ushiriki wa
Mwanamke katika mabadiliko ya Tabianchi kwa sababu wanawake ndio
wanaoathirika zaidi na mabadiliko ya Tabianchi duniani.
Imman
Khatib kutoka YUNA akizugumza kuhusu swala la kupata mafunzo mbalimbali
kuhusu mazingira na mabadiliko ya tabianchi kwa vijana na hasa
wasichana ili wawe na uelewa kuhusu mambo hayo.
Sehemu ya vijana walioshiriki mkutano huo ulioandaliwa na YUNA kwa maslahi ya vijana wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako