Mkurugenzi
wa Benchmark Production, Rita Paulsen aka Madam Rita amesema yeye ni
miongoni mwa wanawake waliopata ujauzito wakiwa na umri mdogo lakini
alikuwa jasiri wa kukabiliana na hali hiyo hadi akafanikiwa.
Kupitia
Facebook, Madam Rita amewashauri wasichana wanaojikuta katika katika
hali hiyo kutokata tamaa kwakuwa bado wanaweza kufanikiwa.
“Jambo
mmoja msilofahamu kuhusu mimi,Nilipata ujauzito nikiwa na umri mdogo
sana. Kwa jamii yetu inayotuzunguka, ukizaa katika umri mdogo, watu huwa
wanakunyanyapaa, hukuona haufai kuwa katika jamii na hata kukuhukumu.
Kwa umri ule niliona ni kama hamna tena maisha kwangu lakini sikukata
tamaa na leo hii ujasiri wangu na kitu kinachonipa msukumo wa maisha
hadi kufika hapa nilipo ni hicho kilichonikuta nikiwa na umri
mdogo.Kukataa tamaa isiwe ndio chaguo lako la kwanza,” aliandika Rita.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako