Imewekwa Desemba 23,2013 saa 2:13 mchana.
Na Oscar Assenga,Korogwe.
JESHI
la Polisi mkoani hapa kwa
kushirikiana na wakazi wa Kijiji cha Maili kumi wilayani Korogwe wamefanikiwa kuwakamata watu saba kwa tuhuma za kuhusika na kuweka mabomu yaliyokuwa yameandaliwa tayari kwa kulipuka kwenye nyumba mbili tofauti za ibada.
kushirikiana na wakazi wa Kijiji cha Maili kumi wilayani Korogwe wamefanikiwa kuwakamata watu saba kwa tuhuma za kuhusika na kuweka mabomu yaliyokuwa yameandaliwa tayari kwa kulipuka kwenye nyumba mbili tofauti za ibada.
Pamoja
na mabomu hao watuhumiwa hao ambao majina yao yanahifadhiwa kwa sababu
za kiuchunguzi wanatuhumiwa kuhusika na kukutwa na vifaa mbalimbali vya
kutengenezea milipuko ya mabomu hayo pamoja na silaha za jadi ambazo pia
zilikuwa zimefichwa katika nyumba hizo za ibada huku katika Kijiji cha
Maili kumi wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.
Watu
hao walikamatwa wakiwa na chupa 10 ambapo tano zilikuwa na Petrol
zikiwa na tambi zake ndani,gololi 103 ambazo hutumiwa kwa
milipuko,galoni kubwa mbili zilizokuwa na lita nne za
petrol,majambia,mishale yenye sumu,soksi za kuzuia
uso(mask)upinde,Daftari lenye mafunzo ya kijeshi kuhusu namna kufungua
na kufunga silaha.
Vifaa
vingine ni mapanga,visu,Mifuko ya Sandarusi ,manati,vifuniko 12 vya
maji,kofia nne na vitambaa vya kufunga kichwani pamoja na Tende
walizokuwa wakitumia kama chakula.
Akizungumza
katika mahojiano na TANGA RAHA BLOG ofisini kwake leo,Kamanda wa Polisi
mkoa wa Tanga Constantine Massawe alisema kuwa watu hao walikamatwa
Disemba 17 mwaka huu majira ya saa 2.00 usiku huko wilayani Korogwe.
Kamanda
Massawe alisema kuwa Askari Polisi wakiwa kaika kizuizi cha Maili 10
wilaya ya Korogwe waliwatilia shaka vijana watatu wa kiume waliokuwa
wamebeba vifurishi na walipotaka wasimame walikimbilia msituni na ndipo
mmoja alipokamatwa na Askari hao.
“sasa
baada ya kukamatwa huyu mmoja na ndipo alipopekuliwa na kukutwa na
vifaa hivyo kwenye begi lake na ndipo msako wa kuwatafuta hawa wengine
ulipoanza”,alisema Kamanda huyo.
Hata
hivyo alisema kuwa alisema kuwa katika msako huo ambao ulifanywa na
Polisi kwa kushirikiana na wananchi wa eneo la Maili kumi ndipo
walipobaini kuwepo kwa vifaa vingine katika nyumba mbili tofauti za
ibada zilizopo Kijijini hapo.
Alisema
watuhumiwa hao baada ya mwenzao kukamatwa walikimbia kujificha kwenye
nyumba hizo za ibada ndipo wakazi wa maeneo hayo walipowatilia mashaka
na kutoa taarifa kwa Polisi.
“Baada
ya kukimbizwa wakaona mahali salama kwao ni kwenye nyumba za ibada
lakini wananchi wa eneo lile waliwatilia shaka na kuamua kutoa taarifa
ndipo yalipokutwa hayo mabomu ambayo yalikuwa yameshaandaliwa kulipuka
kwani kulikuwa na petrol na tambi ndani ya chupa hizo na zile gololi
hutumika kama silaha zinapolipuka”,alifafanua Kamanda Massawe.
Hata
hivyo kwa mujibu wa Kamanda huyo ni kwamba baada ya mahojiano ya Polisi
na watuhumiwa hao walibaini kuwa ni miongoni mwa wale waliokimbi katika
oparesheni ya kuwasaka wahalifu iliyofanyika mwishoni mwa mwezi Novemba
mwaka huu huko wilayani Kilindi.
“Hawa
ni miongoni mwa wale waliosababisha machafuko wilayani Kilindi ambapo
Mgambo aliuawa sasa wengine walikimbia na inaonekana nao hawa wapo
katika mtandao huo”,alisema.
Kamanda
Massawe alitoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Tanga kutoa taarifa mara
moja kwa Polisi mara wanapobaini kuwepo kwa watu ambao wanawatilia
mashaka kwenye maeneo yao.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako