A

A

JOSEPH LUDOVICK AFANYIWA FUJO NA WANACHADEMA KWENYE KONGAMANO LA UHURU-LANDMARK HOTEL

Quote By Joseph Ludovick
Wana mabadiliko,niliwaarifu kuwa nipo kwenye kongamano la uhuru lililoandaliwa na chama chetu pale landmark hotel.nimefika kwa mwaliko rasmi wa muandaaji,Antidius Rweyongeza.nami nilimuuliza kuwa isije ikazuka hoja ya huyu msaliti.akasema hilo ni kongamano la wazi juu ya uhuru wa taifa.nimefika na kuketi huku hotuba zikiendelea.kisha nikataka kuweka taarfa kwa jukwaa.
ndipo mtu mmoja akapita mbele yangu akitaka kunipiga picha.nilimgundua mapema nikaficha sura.haraka nikamwona anakwenda mbele kwa Heche mwenyekiti wa bavicha na kuongea naye.nikapata hisia kuwa kuna jambo linapikwa juu yangu.nikamwambia niliyekaa naye kuwa naona hawa vijana wanatengeneza jambo dhidi yangu kwa hiyo ninaondoka.

hakunielewa.mimi nikaondoka wakati yule aliyekwenda meza kuu hajarudi kuwapa taarifa wenziye.nikapita kwa antidius kiongozi aliyenialika na kumwambia kuwa naona brigade wanaanza kuniwinda kwa hiyo ninaondoka.akasikitika akasema basi kama wewe unaona hivyo,ondoka.nikaondoka,nikapi ta toilet pale hotelini.wakati ninatoka,akaja dada wa chadema akaniita akisema kaka naomba tuonane.nikakataa na kuendelea kuondoka.

yaonekana nikawa nimewa time.nikatoka nje na kuanza kuondoka.naona nyuma yule aliyekuwa meza kuu akarudi.sijui kama alielekezwa au nini.nikiwa nimeshakaribia kwenye daraja la ubungo,nikaona wakili mwanasheria wa bavicha ananikimbilia na kunishika mkono,akisema ninaitwa kule kwenye ukumbi.nikamkatalia.ghafla wakaja kundi la watu kama sita.wakanishika kwa nguvu.nikahoji kwa nini wakasema nimevuruga mkutano.watu arround wakanitetea bali wale vijana wakasema nimeiba kule kwenye mkutano.wakanidhibiti huku wananchi sasa wakiwa hawawezi kunitetea kwani wameambiwa nimeiba kule mkutanoni.

wakaniburuta kurudi ukumbini.hata nilipowaeleza kuwa basi twende,wakakomaa kuniburuta.kisha karibu na ukumbi nikataka kiongozi aliyenialika aitwe.nikauliza pia kama kongamano lilikuwa kikao cha ndani cha chadema.nikaomba viongozi waitwe ili waseme nimefanya jambo gani baya.kiongozi wa vijana wale ,mtu wa makamo,akawashauri waniache niondoke.naam nikaondoka.

sasa nikakuta wameniibia hela zangu elfu 60. nikawa naondoka tu kwa mshangao.kumbe kuna mpango tena wameufanya kunizunguka kwa mbele na kunizushia wizi pale ubungo darajani.nilipofika pale vijana watatu wakanibana wakaanza kushout kuwa nimevuruga mkutano wa chadema pale landmark. nikawa mbogo na kuwaambia wanipeleke polisi.na bahati nzuri akawepo trafiki eneo lile,akaingilia kati.vijana wakasema nimeiba kule mkutanoni.askari akawahoji,nami nikatoa maelezo yangu,kisha akari akaamuru waondoke.

sasa huko ndiko chama chetu kimefikia.hawa wavuta bangi,na wakora kumbe kazi yao kusingizia watu na kujifanya intelijensia ya chama makini.nadhani kama hizi bangi na upumbavu ndiyo inakuwa image ya chama,hakika chama chetu kinakwenda kubaya.ninachojiuliza ni je viongozi ndiyo wamebariki upumbavu huu,au imetokana na wavuta bangi wa red brigade? 
sent by Ludovick Joseph
Jamiiforum

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako