JAJI WARIOBA |
DAR ES SALAAM, Tanzania
Taarifa
iliyotolewa na Katibu wa Tume ya Mabadiliuko ya Katiba, Assaa Rashid,
imesema, Jumatatu ijayo ya Desemba 30, 2013, Tume hiyo itakabidhi rasimu
hiyo kwa Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.
"Tume
inapenda kuwafahamisha wananchi na wadau wengine kuwa hafla ya
kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi itafanyika siku ya
Jumatatu, Desemba 30, 2013 saa 6:00 mchana katika Viwanja vya Karimjee,
jijini Dar es Salaam", taarifa hiyo imesema.
Taarifa
imesema, hafla hiyo pia inatarajiwa kuhudhuriwa na Viongozi wa
Serikali, Vyama vya Siasa, Taasisi za kidini, Asasi za kiraia na
wananchi wa kawaida.
Mwenyekiti
wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba anatarajia kuwakabidhi Waheshimiwa
Marais, ripoti ya mchakato wa Katiba na rasimu ya Katiba.
Rasimu
hiyo ya Katiba imetokana na maoni ya wananchi, viongozi na makundi
mbalimbali waliyowasilisha kwa Tume kupitia njia mbalimbali zikiwemo
mikutano, barua pepe, anuani za posta, Tovuti ya Tume na ukurasa wa facebook wa Tume (Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania).
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako