Jeshi
la Polisi mkoani Morogoro limefanikiwa kukamata gari dogo aina ya
Toyota Spacio likiwa limebeba mwili wa mtu aliefari ambaye alitambulikwa
kwa Jila la Khalid Kitala (47) na kukutwa na kete kadhaa za Madawa ya
Kulevywa tumboni.
Kamanda
wa polisi mkoani Morogoro, Faustine Shilogile amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kusema kuwa walipata taarifa za kuwepo kwa gari
hilo toka kwa wasamalia wema ambao waliliona njiani, ambapo inasemekana
lilikuwa linatokea Mkoani Mbeya kuelekea Dar.
Polisi
wa mkoa wa Morogoro waliweka mtego wao kwenye kituo cha Mikumi na
hatimaye kufanikiwa kukamata gari hilo likiwa na watu watatu ndani
(majina yao yamehifadhiwa),pipi saba za vitu vinavyosadikiwa kuwa ni
dawa za kulevya.
Mwili
huo ulipelekwa hospitali na kufanyiwa uchunguzi na kukutwa na pipi
nyingine kumi na saba tumboni mwa Marehmu huyo na inasemekana mtu huyo
alifariki akiwa Mbeya.
Watu
wote watatu ambapo wawili wanahusika na gari hilo na mmoja ni
mfanyabiashara wa Kariakoo wanashikiliwa na polisi huko Morogoro.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako