Zitto
Kabwe leo ameendelea na ziara yake mkoani Kigoma ambapo kwa siku ya
leo alikuwa wilayani kasulu sehemu ambayo amepokelewa na wanachama wengi
wa Chadema pamoja na wananchi mbalimbali,Mapokezi yalianzia Kilombero kilometa 10 kutoka Kasulu Mjini.
Mapokezi yalianzia ofisi ya Chadema jimbo la Kasulu Mjini ambapo Zitto Kabwe alienda kusaini kabla ya kuendelea na taratibu zingine kisha alienda kuongea na wazee wa Kasulu kwenye ukumbi wa chuo cha TTC,baadae kuelekea moja kwa moja uwanja wa shule ya msingi Kijanamo sehemu ulipofanyika mkutano.
Moja ya vitu vilivyo make Headline leo kwenye mkutano huu ni kitendo cha wazee wa Kasulu kumsimika rasmi u-chifu Zitto Kabwe kutoka jina analolitumia la Zitto Kabwe mpaka kuitwa Wami Bhiyagwa jina lenye sifa ya mtu anayetenda matendo mazuri na kukubalika na watu wengi.
‘Sina namna ya kueleza furaha niliyonayo kwa mapokezi makubwa mliyonipa kasulu,Hii ni salamu tosha wajue na mimi nina kwetu,toka nimefika kilombero mpaka naingia kasulu mjini nimeona nyuso za watu,wazee na kina mama zikiniombea kila la kheri yanayonikuta sasa yapite ili tuendelea kutetea maslahi ya mkoa wetu na nchi yetu na kwa uwezo wa mungu yatapita’.
‘Kwangu mimi mambo yote nayaona kama changamoto ya Maisha,maana yake hata Dhahabu ili iwezekuwa Dhahabu lazima ipite kwenye moto,kwa hiyo haya yanayotokea yananipa nguvu zaidi na anayefikiri kama yananinyong’onyesha asahau,kwa sababu watu wa Kigoma wana sema nguvu ya Mamba kumai,nguvu ya mwanasisasa ni watu na watu ndo nyie’
KMapokezi yalianzia ofisi ya Chadema jimbo la Kasulu Mjini ambapo Zitto Kabwe alienda kusaini kabla ya kuendelea na taratibu zingine kisha alienda kuongea na wazee wa Kasulu kwenye ukumbi wa chuo cha TTC,baadae kuelekea moja kwa moja uwanja wa shule ya msingi Kijanamo sehemu ulipofanyika mkutano.
Moja ya vitu vilivyo make Headline leo kwenye mkutano huu ni kitendo cha wazee wa Kasulu kumsimika rasmi u-chifu Zitto Kabwe kutoka jina analolitumia la Zitto Kabwe mpaka kuitwa Wami Bhiyagwa jina lenye sifa ya mtu anayetenda matendo mazuri na kukubalika na watu wengi.
‘Sina namna ya kueleza furaha niliyonayo kwa mapokezi makubwa mliyonipa kasulu,Hii ni salamu tosha wajue na mimi nina kwetu,toka nimefika kilombero mpaka naingia kasulu mjini nimeona nyuso za watu,wazee na kina mama zikiniombea kila la kheri yanayonikuta sasa yapite ili tuendelea kutetea maslahi ya mkoa wetu na nchi yetu na kwa uwezo wa mungu yatapita’.
‘Kwangu mimi mambo yote nayaona kama changamoto ya Maisha,maana yake hata Dhahabu ili iwezekuwa Dhahabu lazima ipite kwenye moto,kwa hiyo haya yanayotokea yananipa nguvu zaidi na anayefikiri kama yananinyong’onyesha asahau,kwa sababu watu wa Kigoma wana sema nguvu ya Mamba kumai,nguvu ya mwanasisasa ni watu na watu ndo nyie’
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako