A

A

BREAKING NEWSSSS ... MTOTO SULEIMAN RAJAB AFARIKI DUNIA GHAFLA

SULEIMAN RAJABU.
 
******
Na Imelda Mtema
MASKINI! Yule mtoto Suleiman  Rajab aliyeteseka muda mrefu akisumbuliwa na uvimbe mkubwa mguuni huku  mamia ya Watanzania wakijitolea kuchanga fedha kwa ajili ya matibabu  nchini India amefariki dunia ghafla nyumbani kwao Ukonga-Kivule, Dar.
Akizungumza kwa masikitiko makubwa baada ya kifo hicho, baba mzazi wa  marehemu, Rajab Upinde alisema kwamba mtoto wake huyo hakuwa  anasumbuliwa na kitu chochote zaidi ya uvimbe uliokuwa mguuni lakini  alishikwa na ugonjwa wa ghafla na kufariki dunia.

Baba huyo alisema kwamba Kampuni ya Global Publishers kwa  kushirikiana na Hoyce Temu kupitia kipindi chake cha Mimi na Tanzania  kwenye Runinga ya Chanel Ten walifanya jitihada kubwa za kukusanya  michango ambayo ilifanikisha maandalizi ya safari ya matibabu India.
“Naumia sana kwa vile kila kitu kilikuwa tayari. Tulikuwa tunasubiri  siku ya kuondoka tu. Global Publishers na Hoyce wamefanya kazi kubwa  kukamilisha safari ya India lakini ndiyo hivyo Mungu kampenda zaidi  kiumbe wake,” alisema baba huyo kwa uchungu.
Akizungumzia kifo cha mtoto wake, baba huyo alisema kuwa siku ya  tukio Sele aliamka akilalamika kichwa kinamuuma ambapo walimpa dawa za  kutuliza maumivu.
Alisema aliporejea kutoka kazini mkewe alimwambia kuwa Sele alikuwa  akilalama kuwa miguu inawaka moto ambapo alimfuata mwanaye chumbani  ambaye aliomba aitiwe shehe.Shehe alipofika alimuombea na baada ya muda aliwaita wadogo zake na kuwaambia yeye anakufa kwani anajisikia vibaya mno.
Baba  huyo aliendelea kusema kuwa akiwa amekaa nje alisikia mwanaye mwingine  akimuita aingie ndani kwani hali ya Sele ilikuwa imebadilika na  alipoingia alimkuta mwili wote umelegea ambapo aliita majirani ili  wamsaidie, walipoingia ndani walimkuta ameshafariki dunia.Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.
“ Ki  ukweli sikuweza kuamini macho yangu kama mwanangu ndio ameniaga kwani  nilikuwa na ndoto nyingi za kumuona akipona tena na kuwa mzima  kama  walivyo watoto wengine” alisema baba huyo.
Kampuni ya Global Publishers kwa kushirikiana na kipindi cha Mimi na  Tanzania kinachorushwa kupitia Televisheni ya Channel Ten na mwanadada  Hoyce Temu, na kwa watanzania wote walio nje ya nchi kwa kujitahidi  kutoa michango yao Mungu awabariki sana.
VIA GPL

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako